Habari za Punde

Dkt.Abbasi: Sasa ni wakati wa kutatua changamoto za Kisekta

Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi akitoa maagizo kwa Watendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania kuratibu ushiriki wa Wasanii wa Filamu na BASATA kuratibu ushiriki wa Wasanii wa Muziki  katika kazi za serikali kwa lengo la kuepuka mawakala wanaoleta migogoro  miongoni mwao, leo Novemba 30,2020 jijini Dar es Salaam   katika kikao na wakuu wa taasisi zinazosimamia sekta ya sanaa nchini .


Na Anitha Jonas - WHUSM, Dar es Salaam.

Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi amewataka Wakuu wa Taasisi zinazosimamia Sekta ya Sanaa nchi kuandaa mikakati itakayosaidia kukuza na kuendeleza sekta hiyo.

Dkt. Abbasi ametoa kauli hiyo Leo Novemba 30, 2020 Jijini Dar es Salaam katika kikao na viongozi chenye  lengo la kutafuta suluhu ya namna bora ya kuendeleza sekta ya Sanaa nchini.

Katika kikao hicho Katibu Mkuu huyo alisisitiza kuwa Mhe.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli katika hotuba yake mara baada ya kuapishwa na katika ufunguzi wa Bunge pamoja na katika  Ilani  ameeleza lengo la kuendeleza Sekta ya Sanaa.

Akizungumza katika kikao hicho kilichokuwa na Wakuu kutoka BASATA, COSOTA, Bodi ya Filamu na TaSuBa alisisitiza kuwa lazma Sekta ya Sanaa ijipange kuwa na miundombinu mbinu yake ya kisasa itakayoendeleza kazi hiyo ikiwemo ujenzi wa "sport arena".

"Sasa ni wakati wa kuangalia namna ya kutatua changamoto za kisekta na siyo changamoto  binafsi tuangalie mambo gani yaboreshwe kama ni Sera, Sheria au Kanuni"alisema Dkt.Abbasi. 

Pamoja na hayo Dkt. Abbasi alitoa maagizo mbalimbali  kwa Wakuu hao ikiwemo kuandaa mpango wa kutoka mafunzo mbalimbali, na kwa  TaSUBa  kujipanga kuwa na kozi za muda mfupi utoaji zitakazosaidia  wasanii. 

Vilevile  Katibu Mkuu huyo alitoa maagizo kwa Bodi ya Filamu kusimamia na  kuratibu shughuli zote za Serikali zitakazohitaji na Wasanii Wafilamu na kwa upande wa Muziki BASATA nao ndiyo kuwa waratibu hii ni kwa lengo la kuondoa mawakala miongoni mwao ambao huchangia kuleta changamoto mbalimbali.

Aidha, Dkt. Abbasi pia ameitakaTaasisi ya COSOTA kutafuta mfumo bora wa kieletroniki utakaosaidia ukusanyaji wa mapato ya kazi za wasanii pamoja na namna bora ya kutumia mifumo ya kidijitali katika kulinda haki za wasanii ili waweze kufaidika na kazi zao.

Kwa upande wa Mtendaji Mkuu COSOTA  Doreen Sinare alimshukuru Katibu Mkuu huyo kwa kupata wadau  kutoka India, ambao watashirikiana na wasambazi wa kazi za Filamu Tanzania ambao wanafanya tafsiri ya filamu za kihindi ili kupata ridhaa ya Wamiliki wa Filamu za india zifanyiwe tafsiri

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.