Habari za Punde

Mbunge wa Jimbo la Kiwani Pemba Akabidhi Gari ya Wagonjwa

MBUNGE wa Jimbo la Kiwani Wilaya ya Mkoani Rashid Abdalla Rashid kushoto akimkabidhi ufunguo wa gari ya kuwabeba wagonjwa ya jimbo hilo, katibu wa CCM mkoa wa Kusini Pemba Mohamed Ali Khalfa, ikiwa ni miongoni mwa ahadi alizozitoa kwa wananchi wajimbo hilo wakati wa kuomba kura.
KATIBU wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Kusini Pemba Mohamed Ali Khalfan, akiendesha gari ya kubebea wagonjwa mara baada ya kukabidhiwa na Mbunge wa Jimbo la Kiwani, ili kutoa huduma kwa wananchi wa jimbo hilo.
MBUNGE wa Jimbo la Kiwani Kushoto Rashid Abdalla Rashd, akiangalia gari ya kubebea wagonjwa wa jimbo hilo wakati ikijaribiwa kwa mara ya kwanza baada ya kukabidhiwa kwa uongozi wa jimbo hilo.

KATIBU wa CCM Mkoa wa Kusini Pemba Ndg.Mohamed Ali Khalfan, akimkabidhi ufunguo wa gari ya kubebea wagonjwa Mwenyekiti wa Jimbo la Kiwani Omar Juma Kheri, gari hiyo iliyotolewa na mbunge wa jimbo hilo.

(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA) 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.