Habari za Punde

Si sahihi kwa wanandoa kuwatishia talaka wake zao pindipo wasipochagua wanaotaka wao - Wito

Miongoni wa mwashiriki wa mkutano huo wa siku moja uliokua na lengo la kujadili nafasi ya mwanamke katika uongozi nachangamoto wanazokutana nazo.

 Mshiriki wa majadiliano hayo kutoka ZAFAYCO Shadida Omar Ali akiwasilisha ripoti iliolenga kutazama nafasi za wanake katika uongozi.


 

 Muhammed Khamis-Tamwa Zanzibar

 

Licha ya kumalizika kwa uchaguzi mkuu Zanziabr uliofanyika mwezi Oktoba inalezwa kuwa katika uchaguzi huo na nyenginezo  zilizowahi kupita   kumekuepo kwa baadhi ya wanandoa kuwalazimisha wake zao kuwachagua viongozi wanaowataka wao kinyume na sheria ambayo imeweka wazi kuwa kila mtu ana haki ya kumchagua anaempenda.

 

Taarifa ya uwepo wa mazingira hayo imebuka kufuatilia majadiliano ya baadhi ya viongozi wa dini na washiriki kutoka asasi mbali mbali za kirai visiwani hapa katika mkutano maalumu ulioandaliwa na Tamwa-Zanzibar katika ukumbi wa watu wenye ulemavu kikwajuni mjini Unguja.

 

Akizungumzia suala hilo Sheikh Khamis Abdilhamid  alisema mchakato wa kura na uhuru wa kuchagua haukuanza leo bali umeanza tangu enzi za Mitume hivyo hakuna kitu kigeni ambacho kingeweza kuwapa nguvu zaidi wanaume kuwaamulia wake zao.

 

Alisema uhuru wa kuchagua ni haki ambayo ipo katika kila sehemu na hata enzi za Nabii Yunnus alipigiwa kura na kuchaguliwa yeye awe sehemu ya kutoswa baharini na kila mtu aliheshimua maamuzi ya kura hio licha ya kuwa alieamuliwa alikua Mtume wa Mwenyezimungu lakini hakuna mtu alielazimishwa kumchagua mwengine baada ya yeye.


Alisema wapo baadhi ya wanandoa wamefika mbali zaidi kuwatishia wake zao talaka na wapo wengine ambao wamewahi kuwaacha kabisa wake zao kutokana na tofauti za kisiasa.

 

Kutokana na mazingira hayo alisema si sahihi kwa wanandoa kuwatishia talaka wake zao pindi wasipowachagua wale wanaowataka wao na kwamba kufanya hivyo ni kosa na hakutakua na  talaka inayosihi kwa mazingira hayo.

 

‘’Ni lazima watu wafahamu kuwa si kila talaka hutundikwa kuna mambo mengine mwanamke hawezi kuachika kwa sababu tu mume wake kasema akifanya kitu fulani atakua amemuacha bila kitu hicho kutokua na msingi amba uzito’’aliongezea.

 

Akitolea mfano zaidi  Sheikh Khamis alisema iwapo mume atamkataza mke wake asiende kuhiji Makka na pindi akienda kufanya hija hio atakua ameachika na mke akikataa amri hio hatakua mwneye kuachika kwa kuwa anchokifa nya ni jambo la kheri na lenye manufaa kwake.

 

Awali akiwasilisha  ripoti hio ya utekelezaji  Laila Khamis Jumbe   kutoka Chama cha Wanasheria Wanawake Zanzibar (ZAFELA)  alisema hali hio walikutana nayo katika eneo la kusini  Unguja pamoja na baadhi ya maeneo katika wilaya ya kati.

 

Alisema hadi sasa baadhi ya wanandoa wamekua wakiwalazimisha wake zao kuwachagua wale wanaowapenda wao na sio kutoa fursa kwa mwanamke kumchagua kiongozi anaempenda yeye.

 

Alisema baadhi ya waume kwenye ndoa zao huwaongoza wake zao hadi vituo vya kupigia  kura na hudai kuwa wanataka kuwasaidia na kwakuwa baadhi ya wanawake wanakua na hofu hukubali kusaidiwa licha ya kuwa ana uwezo wa kupiga kura wenyewe.

 

Omar Ali  Khamis kutoka Wilaya ya Kaskazini B Unguja alisema hali hio haipo katika mkoa wa kusini pekee badala yake hata mkoa wa kaskazini Unguja kuna idadi kubwa ya matukio ya aina hio.

 

Alisema katika mkoa wa kaskazini zipo hata baadhi ya ndoa zilivonjika kwa mke kukataa kutii amri ya mume wake katika maamuzi ya kuchagua viongozi wanaowapea wao.

Akizungumza kwa niaba ya tume ya uchaguz Zanzibar (ZEC) mkuu wa divisheni ya mipango Lutfia Faida Haji alisema kuna tatizo kubwa kwa baadhi ya wanaume kwneye ndoa zao n ahata kwenye vyama vya siasa.

 

Alitolea mfano kamati ya maadili ya tuume hio ambayo huundwa na washiriki kutoka vyama vya siasa alisema mara nyingi vyama hivyo vimekua vikipeleka majina ya wanaume kama wajumbe washiriki na sio wanawake.

 

Alisema kwa mazingira hayo bila shaka anaafikiana na washirki wa warsha hio kuwa wamekuepo baadhi ya wanaume huwalazimisha wake zao kuchagua wale wanaowapenda wao jambo ambalo ni kinyume na sheria.

 

Alisema kila mtu anapaswa kuwa huru kumchagua anaemtaka bila kushurutishwa na yoyote yule na kuwataka wanaume kwenye ndoa kutowafanya wanawake kama watu wasiokua na haki ama kufanya maamuzi kwa mustakbali wanaouamini wao.

 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.