Habari za Punde

Tatueni changamoto za wananchi kwa wakati-Kadio

 

Mwenyekiti wa Baraza Dogo la Wafanyakazi Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Emmanuel Kayuni akizungumza na wajumbe wa Mkutano wa Baraza Dogo la Wafanyakazi wa wizara hiyo (hawapo pichani), kushoto ni Katibu Mkuu wa wizara hiyo Christopher Kadio na kulia ni Katibu wa Baraza hilo, Francis Lubeti  mkutano huo umefanyika jijini Dodoma
Mjumbe wa Baraza Dogo la Wafanyazi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Abas Malekela akizungumza wakati wa kikao cha baraza hilo kilichofanyika jijini Dodoma.
Mjumbe wa Baraza Dogo la Wafanyazi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Kamishna wa Polisi, Albert Nyamhanga akizungumza wakati wa kikao cha baraza hilo kilichofanyika jijini Dodoma.

Na Mwandishi Wetu                                                                                                                                          Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Christopher Kadio, amewaagiza wafanyakazi wa Wizara hiyo kutatua kwa wakati changamoto za wananchi wanaofika kutoka sehemu mbalimbali kuja kupata huduma wizarani.

Akizungumza jijini Dodoma wakati wa kufungua Mkutano wa Baraza Dogo la Wafanyakazi wa wizara hiyo, Katibu Mkuu Kadio amewataka wajumbe wa mkutano huo kwenda kufanya kazi kwa weledi ili kuwasaidia wananchi katika kutoa huduma iliyo bora.

Alisema wananchi wanapopeleka changamoto zao ni wajibu wao kuzitatua na kuwarudishia kwa wakati kwa sababu ni wajibu wao kufanya kazi hizo.

“Nyie wajumbe wa Baraza mkawe mfano wa kuigwa katika vitengo vyenu vya kazi, masuala mliyojadili katika mkutano wa Baraza mkawape elimu wenzenu waliowachagua kuwawakilisha” alisema Kadio

Kadio pia   aliwapongeza viongozi waliochaguliwa katika Baraza hilo na kuwataka kwenda kuwa mfano bora katika maeneo yao ya kazi.

Alisema watumishi wenzenu wana Imani kubwa na nyie hivyo nanyi mkafanye kazi ya kutathmini mtumishi mmoja mmoja ili kuboresha mazingira yao ya kazi kwa ujumla.

Alifafanua zaidi mkajenge utaratibu wa kukutana na menejimenti ya wizara ili kushauri namna ya kuweka mikakati bora ya ufanyaji kazi kwa watumishi.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.