Meneja wa Ezypesa Nuirat Zahor akiwafahamisha mawakala jinsi ya
kutoa huduma kwa Wateja katika kongamano la mawakala lililofanyika jana
Unguja-Zanzibar.Mawakala hao walihimizwa kuzingatia sheria na taratibu za
utoaji wa huduma hiyo ili kuleta tija zaidi.
·
Yahimiza kuzingatia sheria ili huduma hiyo iwe na tija
kwa Taifa.
Zanzibar.
Kampuni ya simu za mkononi Zantel, imeendesha mafunzo kwa mawakala wake
na kuwataka mawakala wa kampuni hiyo kuhakikisha wanafuata sheria na taratibu
za nchi katika ufanyaji wa kazi zao ili waweze kuleta tija hapa nchini.
Wito huo ulitolewa na Meneja wa Kusimamia utaratibu wa
Biashara Salum Mussa Haji alipokuwa katika mkutano na mawakala uliofanyika huko
Kiembesamaki.
Alisema hatua hiyo itasaidia kufikia malengo ya
kufanya biashara hizo kwa kuweza kuinua kipato chao na taifa kwa ujumla.
Meneja huyo alisemaa kampuni hiyo inawajibu mkubwa wa
kuweka mazingira salama kwa wafanyabiashara hao ili kuona wanatekeleza majukumu
yao kwa kufuata sheria za nchi.
Alisema lengo la mkutano huo ni kuwakumbusha mawakala
hao kufahamu vitu vinavyohitajika katika uendeshaji wa biashara zao ikiwemo
kukata leseni pamoja na kufuata taratibu nyengine za nchi.
Kwa upande wa Meneja wa Masoko na Mawasiliano wa Kampuni
hiyo, Rukia Mtingwa, alisema mkutano huo wanafanya kila mwaka kwa mawakala wao
ili kusaidia kutatua changamoto zinazowakabili pamoja na kuleta ufanisi katika
utekelezaji wa wajukumu yao.
Alisema mawakala hukutana na changamoto kadhaa katika
kazi zao ambazo husababisha kutofikia malengo yao hivyo kupitia kongamano hilo
husaidia kutoa mchango mkubwa wa kutatua changamoto hizo.
Kwa upande wa afisa wa huduma ya Ezypesa Eunice
Hubert, alisema kampuni hiyo imekuwa ikitoa huduma tofauti ili kuwarahisishia
wananchi kuzitumia kwa urahisi pamoja na kuwaondoshea usumbufu.
Hivyo alitumia fursa hiyo kuitaka jamii kuzitumia
huduma zinazotolewa na kampuni hiyo ili waweze kunufaika nazo na kuleta
maendeleo pamoja na kukuza uchumi wan chi.
No comments:
Post a Comment