Habari za Punde

KAMATI ZA ULINZI WA MWANAMKE NA MTOTO 16343 ZAANZISHWA

Mkuu wa Wilaya ya Butiama AnnaRose Nyamubi (kushoto) akizungumza na timu maalum ya utaoji wa Mafunzo kwa Kamati ya ulinzi kwa Mwanamke na Mtoto Kitaifa ikiongozwa na Mkurugenzi Msaidizi idara ya Maendeleo ya Jinsia Grace Mwangwa (kulia) ilipofika ofisini kwake Wilayani Butiama.


Na Mwandishi Wetu Butiama Mara

Inaelezwa kuwa jumla ya Kamati za Ulinzi kwa Mwanamke na Mtoto 16343 zimeanzishwa katika mikoa Halmashauri, Kata na Vijiji ili kuongeza nguvu katika mapambano dhidi ya vitendo vya ukatili wa kijinsia dhidi ya Wanawake na Watoto.

Hayo yanesemwa Wilayani Butiama mkoani Mara na Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Maendeleo ya Jinsia kutoka Wizara ya Afya- Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Grace Mwanga wakati wa mafunzo kwa kamati ya ulinzi ya Mwanamke na Mtoto ya Halmashauri hiyo.

Grace amesema kuwa Serikali kupitia Wizara ya Afya- Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii imeweza kuratibu mafunzo kwa Kamati hizo kwa kushirikiana na Shirika la UNFPA ili kuzipa nguvu Kamati hizo katika kutekeleza majukumu yake.

Ameongeza kuwa Wizara inatekeleza Mpango wa Kitaifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA) unaolenga kupambana na kutokomeza vitendo vya ukatili kwa asilimia hamsini nchini.

Akifungua Mafunzo kwa Kamati ya ulinzi wa Mwanamke na Mtoto ya Halmashauri ya Wilaya ya Butiama, Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe. AnnaRose Nyamubi amekema vitendo vya ukatili wa kijinsia hasa ukeketaji na mimba za utotoni vinavyokatisha ndoto za watoto hasa wa kike za kuendelezwa katika kupata elimu.

Ameongeza kuwa Wilaya ya Butiama imejipanga katika kuhakikisha inapambana na vitendo vya ukatili wa kijinsia katika maeneo yao kwa kushirikiana na wajamii husika wakiwemo wazee wa mila, watu mashuhuri na viongozi wa dini ili kuhakikisha vitendo vya uaktili dhidi ya wanawake na watoto vinatokomea.

Naye Mbunge wa Jimbo la Butiama Mhe. Jumanne Sagini anasema nguvu ya viongozi wa kisiasa inahitajika katika kuhakiksha wanahusika katika mapambano dhidi ya vitendo vya ukatili.

“Sisi viongozi wa siasa tuwajibike kwa nafasi zetu tuoaze sauti kupinga vitendo vya kikatili dhidi ya wananwake na watoto kwani inawezekana tukiamua kwa pamoja” alisema

Naye Mchungaji wa Kanisa la EAGT Butiama Joseph Mgabu amesema kuwa viongozi wa kidini wana jukumu kubwa sana katika mapambano dhidi ya vitendo vya kikatili hasa katika kutoa elimu kwa waumini wao katika nyumba za ibada amnayo itasaidia jamii kujua madhara ya vitendo hivi.

Kwa upande wake Bi. Hesha Kisibo ameiomba jamii kuachana na mfumo dume unaowakandamiza na kuwanyimwa wasichana na wanawake haki zao hivyo kusababisha kutokea kwa vitendo vya kikatili.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.