Habari za Punde

Mafunzo ya kuwajengea uwezo Walimu juu ya namna ya kuwafundisha watoto masuala ya virusi vya Ukimwi

 Na Maulid Yussuf WEMA


Mkurugenzi Idara ya Mafunzo ya Ualimu, bi Maimuna Fadhil Abbas amesema kuna umuhimu wa kupewa taaluma na kuwajengea uwezo kwa Walimu katika masuala mbalimbali ili kukuza uelewa wao na kuweza kutoa elimu kwa watoto.

Akifungua mafunzo ya kuwajengea uwezo Walimu juu ya namna ya kuwafundisha watoto masuala ya virusi vya Ukimwi na ukimwi pamoja na stadi za maisha, katika ukumbi wa kituo cha Walimu TC Kiembe samaki Mjini Unguja, bi Maimuna amesema hali hiyo itawasaidia watoto kujitambua kijinsia pamoja na kuweza kukabiliana na changamoto mbalimbali ikiwemo za udhalilishaji.

Amesema bado kuna watoto hawajitambui kutokana na wazazi kuwa na aibu ya kuwaficha watoto wao na kutokuwa karibu nao katika kuwapa stadium za maisha na kujitambua.

Amesema taaluma ya uzazi salama na afya pamoja na virusi vya ukwi na ukimwi, inapaswa kutolewa kwa jinsia zote sio kwa wanawake pekee, kwani kuna uwezekano mkubwa wa kuweza kuweza kusaidiana katika hali mbalimbali katika mzunguko wa maisha yao.

Amewataka Walimu hao kutumia  SITIARI au lugha nzuri katika kuwafundisha watoto hao juu ya masuala hayo na sio kuficha hali ambayo kwani haitawasaidia katika kujua namna ya kujilinda afya zao hasa kipindi wanachoanza kupata ukubwa.

Amesema, wameamua kuwapa mafunzo hayo walimu wa madarasa kutokana na wao ndio wahusika wakuu wa kuwa karibu na watoto kwa kuweza kuwapa ushauri nasaha watoto juu ya dhana nzima ya kuweza kujikinga na matatizo mbalimbali ikiwemo masuala ya ubakaji, udhalilishaji na kujitambua na kuwafanya Wanafunzi wao kuwa huru wa kuweza kuwaambia matatizo mbalimbali yanayowakabili.

Aidha amesema kuwa Walimu wana wajibu mkubwa wa kuwalinda na kuhakikisha wanawapa elimu bora watoto wao katika mazingira yote wakiwa  Skuli na hata nyumbani na kuwazoeaha kusema HAPANA, ili kuwakinga na vitendo mbalimbali ikiwemo ya udhalilishaji.

Hata hivyo amesema walimu bado wanahitaji mafunzo kuhusu masuala ya Elimu ya uzazi, hivyo ameishukuru UNESCO kwa kuona umuhimu wa kutoa elimu hiyo na kujitolea kufadhili pamoja na kuwashukuru walimu kwa kuitikia wito juu ya Mafunzo hayo.

Nae Afisa wa Elimu na Afya kutoka Shirika linaloshughulikia masuala ya Elimu Sayansi na Utamaduni, UNESCO Zanzibar bi Hasina Salim Bukheti amesema mafunzo hayo yanafanyika kupitia mradi wa O3s yaani Our rights ambayo ni haki za mtoto, Our life ambayo ni maisha ya mtoto na  Our futer, ambayo inaangalia mustakbali mzima wa mtoto n kijana katika masuala ya Afya Na elimu.

Amesema mradi huo wa O3s  una  lengo la kuwasaidia watoto kuweza kuwajengea mustakbali mzima wa afya ya uzazi salama, kuwa imara, kuwapa taarifa sahihi za kijinsia ili aweze kujilinda, kujiamini na kusimamia vizuri haki zake za msingi na kupata maisha mazuri hapo baadae.

Amesema Mradi huo pia  unasimamia Yale ambayo yamepangwa na Wizara ya Elimu kupitia Sera iliyopo juu ya masuala mtambuka ambayo yanawakabili watoto katika njia mbalimbali ambayo yanawaharibia maisha yao na kuwafanya kutofanya vizuri katika masomo yao.

Kwa upande wake Afisa Mafunzo ya Ualimu kutoka Idara ya Mafunzo ya Ualimu Zanzibar Mw. mohammed Ali Mohammed (mwalimu Ugoda) amessma lengo la mfunzo hayo ni kuwajengea uwezo Walimu wa kuweza kufundisha Elimu ya Afya ya uzazi, masuala ya virusi vya ukimwi na ukimwi, stadi za maisha pamoja na masuala ya jinsia.

Amesema hatua hiyo imekuja kutokana na utafiti waliiufanya kwa walimu wao nankuoa kuwa walimu wengi hawana uwezo wa kufundisha masuala hayo katika Skuli zao pamoja na wengine kutojiamini wakati wa kufundisha masuala hayo ambayo ni muhimu katika Skuli kwa wakati wa Huu unaoendelea.

Mafunzo hayo ya siku tatu yamewashirikisha walimu kutoka Skuli mbalimbali za maandalizi na msingi, yameandaliwa na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali chini ya Ufadhili wa UNESCO.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.