Habari za Punde

Mbunge wa Jimbo la Welezo aungana na wananchi kufanya usafi wa mazingira jimboni kwake

BAADHI ya Wananchi wa Shehia za Mchikichini na Hawai wakifanya usafi katika maeneo yao kwa kushirikiana na viongozi wa Baraza la Manispaa ya Magharibi 'A' na Viongozi wa Jimbo la Welezo.(PICHA NA IS-HAKA OMAR).
BAADHI ya Wananchi wa Shehia za Mchikichini na Hawai wakifanya usafi katika maeneo yao kwa kushirikiana na viongozi wa Baraza la Manispaa ya Magharibi 'A' na Viongozi wa Jimbo la Welezo.(PICHA NA IS-HAKA OMAR).
BAADHI ya Wananchi wa Shehia za Mchikichini na Hawai wakifanya usafi katika maeneo yao kwa kushirikiana na viongozi wa Baraza la Manispaa ya Magharibi 'A' na Viongozi wa Jimbo la Welezo.(PICHA NA IS-HAKA OMAR).
MBUNGE wa Jimbo la Welezo Mhe.Maulid Saleh Ali (kulia) akisukuma bero la taka kwa ajili ya kwenda kuzihifadhi katika eneo maalum la taka, katika zoezi la usafi wa mazingira lililofanyika leo katika Shehia za Hawai na Mchikichini ndani ya Jimbo la Welezo Zanzibar.


NA IS-HAKA OMAR,ZANZIBAR.

MBUNGE wa Jimbo la Welezo Mhe.Maulid Saleh Ali,amewataka wananchi wa jimbo hilo kuendeleza utamaduni wa kufanya usafi wa mazingira katika maeneo yao ili kuepuka maradhi ya miripuko.

Wito huo ameutoa leo mara baada ya kushiriki kampeni maalum ya usafi wa mazingira iliyofanyika katika shehia za Hawai na Mchikichini jimboni humo alisema kila mwananchi ana jukumu la kufanya usafi katika eneo analoishi ili kudumisha dhana ya usafi kwa vitendo.

Alisema kwa kushirikiana na uongozi wa jimbo atahakikisha suala la usafi linapewa kipaumbele kinachositahiki ili shehia zote ziwe safi muda wote.

Aliahidi kwamba atatoa vifaa vya kisasa vya kusafisa mazingira vikiwemo mifagio,mapanga na ndoo maalum za kuifadhia takataka ili kuweka mazingira ya jimbo hilo katika hali ya usafi.

Pamoja na hayo aliwasihi vijana mbalimbali wa jimbo hilo kuanzisha vikundi vya kufanya usafi ili visaidie kufanya usafi sambamba na kulinda mazingira ya jimbo hilo yasiharibiwe.

''Wito wangu kwa wananchi wote wa Jimbo hili ni kwamba kila mtu kwa nafasi yake bila kujali cheo na wadhifa wake sote tushirikiane katika kufanya usafi wa mazingira kwani faida ya kufanya hivyo ni kubwa zaidi kuliko kuacha kila eneo likatupwa taka.'', alisema Maulid.

Naye Kaimu Mkurugenzi wa Baraza la Manispaa ya Magharibi ''A'' Amour Ali Abdallah,amesema kwa upande wa manispaa hiyo wamejipanga kushirikiana na masheha mbalimbali kutoa elimu kwa wananchi juu ya umuhimu wa kudumisha usafi na ulinzi wa mazingira.

Alisema pamoja juhudi za shehia hiyo ya Hawai kuandaa siku maalum ya ''shehia day'' kwa ajili ya kuhamasisha masuala ya usafi katika maeneo hayo bado wananchi hawajahamasika kushiriki kikamilifu katika utekelezaji wa kampeni hiyo.

Alisema shehia mbalimbali za manispaa hiyo zinakabiliwa na tatizo la ukosefu wa maeneo maalum ya kutupa takataka jambo ambalo litafutiwa ufumbuzi wa kudumu na manispaa hiyo.

Aidha Kaimu Mkurugenzi huyo Amour, alisema kampeni hiyo ya kufanya usafi wa maeneo mbalimbali ya shehia hizo unatakiwa kuwa endelevu na kuzitaka shehia zingine za manispaa hiyo kuiga kwani ni utaratibu mzuri unaosaidi kuweka mazingira katika hali ya usafi.

Alisema Manispaa hiyo itaanza zoezi la kukagua usafi nyumba kwa nyumba na wananchi wakaobainika wanaishi katika mazingira machafu watatozwa faini sambamba na kuchukuliwa hatua kali za kisheriA.

''Mheshimiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi, anasisitiza nchi iwe katika hali ya usafi sasa na sisi lazima katika ngazi zetu tutekeleze agizo hilo kwa kuhakikisha mitaa yote na maeneo mbalimbali ya manispaa yetu yanakuwa safi muda wote.'', alisisitiza Amour.

Naye Mstahiki Meya wa Manispaa hiyo Choum Shuwari Machano,aliwapongeza wananchi waliojitokeza kushiriki katika zoezi hilo la usafi ambalo linagusa maisha ya kila mwananchi.

Aliwasihi wananchi hao kuendeleza utamaduni wa kufanya usafiri katika maeneo yao bila ya kusubiri watendaji wa Manispaa kwani suala la usafi linawahusisha watendaji wote.

Akizungumza Sheha wa Shehia ya Mchikichini Kijakazi Ferouz Khamis,alisema wanaendelea kuwahamasisha wananchi wajitokeze kwa wingi kufanya usafiki katika maeneo yao.

Naye Mkaazi wa Shehia hiyo Asha Seif Salum, aliomba Manispaa ya Magharibi ''A'', kufanya kutenga maeneo maalum ya kutupa taka ili kuepusha taka hizo kusambaa mitaani.
 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.