Habari za Punde

Mkurugenzi Mkuu ZAECA azungumza na wanahabari wamefanikiwa kuokoa fedha za miradi mbali mbali ya Umma


Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia Rushwa na Uhujumu Uchumi Zanzibar Mussa Haji Ali akitoa taarifa kwa Umma juu ya utendaji kazi wa ZAECA  huko Ofisini kwake Mnazimmoja Zanzibar 


PICHA NA FAUZIA MUSSA /MAELEZO ZANZIBAR.

Mwashungi Tahir     Maelezo      10-12-2020.

Mamlaka ya ya kuzuia Rushwa na Uhujumu wa Uchumi Zanzibar ZAECA imefanya ufatiliaji wa matumizi mbali mbali ya fedha za Umma kwa lengo la kuhakikisha fedha zote za miradi zinatumika kama zilivyopangwa.

Akizungumza na waandishi wa habari Mkurugenzi wa wa mamlaka ya kuzuia rushwa na uhujumu wa uchumi Zanzibar ZAECA Mussa Haji  Ali  huko katika ukumbi wa ZAECA ulioko Vuga wakati alipokuwa  akitoa taarifa kwa umma juu ya utendaji wa kazi za ZAECA .

Amesema ufatiliaji wa fedha za umma zinazotumika katika miradi mbalimbali una lengo la kuhakikisha kwamba hakuna aina ya ubadhirifu ambao unatokea katika matumizi hayo na sheria zinafuatwa ikiwemo sheria ya matumizi ya fedha za umma na ya manunuzi.

Hivyo amesema ZAECA  imefanikiwa kuokoa fedha katika miradi mbali mbali ya umma pamoja na kurejesha fedha kwa wanajamii ambazo zilitumika kinyume na sheria , kanuni na taratibu za matumizi ya fedha za umma.

Aidha alisema Serikali ya awamu ya nane katika mapambano ya dhidi ya rushwa na uhujumu wa uchumi nchini, ZAECA imefanya ufatiliaji wa miradi mbali mbali ya maendeleo inayotekelezwa na Taasisi za umma ili kuhakikisha inatekelezwa kwa viwango na kwa wakati .

 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.