Habari za Punde

Rais Dk Hussein Mwinyi ashiriki maziko ya Marehemu Mwanakombo Haji Omar

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk. Hussein Ali Mwinyi akijumuika na Waumini wa Kiislam katika Sala yakuusalia mwili wa Marehemu Mwanakombo Haji Omar  ikiongozwa na Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh. Saleh Omar Kabi, iliofanyika katika Msikiti wa Mikunguni na (kulia kwa Rais) Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk. Hussein Ali Mwinyi na (kulia kwake) Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman Abdulla na Naibu Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh. Othman Hassan, akisoma dua baada ya kumaliza kwa Sala ya kuusalia mwili wa marehemu Mwanakombo Haji Omar, ilifanyika katikaMsikiti wa Mikunguni Jijini Zanzibar.leo 22/12/2020.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi na (kulia kwake) Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman Abdulla na (kushoto kwa Rais) Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Mhe. Rashid Hadid Rashid, wakijumuika na Wananchi katika maziko ya Marehemu Mwanakombo Haji Omar, yaliofanyika Kijijinikwao Uzini Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja yaliofanyika leo 22/12/2020.(Picha na Ikulu)
/RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk. Hussein Ali Mwinyi, akisalimiana na Bw. Omar Haji, baada ya kumalizika kwa maziko ya Marehemu Mwanakombo Haji Omar, yaliofanyika katika Kijiji cha Uzini Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja leo 22/12/2020.(Picha na Ikulu)
 

1 comment:

  1. Assalam Alaykum ndugu Mapara,

    Tungependa kujua huyu Marehemu Mwanakombo Haji Omar no Nani?

    Ingepe deza taarifa zikaongezwa nyama kidogo ili zifahamike na kupunguza maswali.

    Shukrani sana

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.