Habari za Punde

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira akutana na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa  Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Ummy Mwalimu akiwa katika picha ya pamoja na  Makamu wa Kwanza wa Rais Mhe. Maalim Seif Shariff Hamad mara baada ya mazungumzo  hii leo Visiwani Zanzibar, Waziri Mwalimu yuko Zanzibar kwa lengo la kujitambulisha

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa  Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Ummy Mwalimu akiteta jambo na  Makamu wa Kwanza wa Rais Mhe. Maalim Seif Shariff Hamad mara baada ya mazungumzo  baina yao hii leo Visiwani Zanzibar.

Na Lulu Musa 

Waziri Ummy Mwalimu amefanya mazungumzo na Makamu wa Kwanza wa Rais Maalim Seif Sharrif Hamad Chukwani Zanzibar.

Mhe. Hamad amesisitiza umuhimu wa Wizara zenye hoja za Muungano kukutana na kutafuta suluhu ya mapema na kuhamasisha  Wizara zisizo na hoja kukutana pia kwa lengo la kudumisha undugu baina ya  Tanzania bara na Tanzania Zanzibar.

“Nashauri na kusisitiza Wizara zinazoshabihiana zikutane na kuhakikisha hoja zinazopatiwa ufumbuzi zitekelezwe ipasavyo” alisisitiza Maalimu Seif Sharif Hamad.

Waziri Ummy Mwalimu yuko visiwani Zanzibar kwa ziara ya kikazi ya siku mbili na hapo kesho atatembelea miradi ya Muungano inayotekelezwa pande zote mbili.

1 comment:

  1. INAPENDEZA SANA KUIMARISHA MUUNGANO BADALA YA KUUZODOA NA KUFIKIRIA KUANZA MAMBO UPYA BARA NA VISIWANI

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.