Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Ummy
Mwalimu akiwa katika picha ya pamoja na Makamu
wa Kwanza wa Rais Mhe. Maalim Seif Shariff Hamad mara baada ya mazungumzo hii leo Visiwani Zanzibar, Waziri Mwalimu yuko
Zanzibar kwa lengo la kujitambulisha
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Ummy
Mwalimu akiteta jambo na Makamu wa
Kwanza wa Rais Mhe. Maalim Seif Shariff Hamad mara baada ya mazungumzo baina yao hii leo Visiwani Zanzibar.
Na Lulu Musa
Waziri Ummy Mwalimu amefanya mazungumzo na Makamu wa Kwanza wa Rais Maalim Seif Sharrif Hamad Chukwani Zanzibar.
Mhe. Hamad amesisitiza umuhimu wa Wizara
zenye hoja za Muungano kukutana na kutafuta suluhu ya mapema na kuhamasisha Wizara zisizo na hoja kukutana pia kwa lengo la
kudumisha undugu baina ya Tanzania bara na
Tanzania Zanzibar.
“Nashauri na kusisitiza Wizara zinazoshabihiana
zikutane na kuhakikisha hoja zinazopatiwa ufumbuzi zitekelezwe ipasavyo”
alisisitiza Maalimu Seif Sharif Hamad.
Waziri Ummy Mwalimu yuko visiwani Zanzibar kwa ziara ya kikazi ya siku mbili na hapo kesho atatembelea miradi ya Muungano inayotekelezwa pande zote mbili.
INAPENDEZA SANA KUIMARISHA MUUNGANO BADALA YA KUUZODOA NA KUFIKIRIA KUANZA MAMBO UPYA BARA NA VISIWANI
ReplyDelete