Habari za Punde

Mkadarasi wa Skuli ya Kibuteni Mkoa wa Kusini Kukamilisha Kwa Ujenzi wa Skuli Hiyo Kama Makubaliano Yanavyosema.

Na Maulid Yussuf WEMA

Katibu mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Dkt. Idrissa Muslim Hija, ameitaka kampuni ya ujenzi wa Skuli ya Sekodari Kibuteni kuhakikisha matengenezo yote waliyokubaliana kuyakamilisha kwa muda waliokubaliana.

Amesema kufanya hivyo kutasaidia kuwaweka salama katika kazi zao pamoja na Wizara nayo kuwa katika hali nzuri.

Akizungumza wakati aliposaini makabidhiano ya Skuli ya Sekondari Kibuteni baada ya kukagua na kuridhishwa na majengo hayo, amesema majengo hayo yanatarajiwa kufunguliwa mapema mwakani.

Amesema kukamilika kwa ujenzi wa Skuli hiyo kutawasaidia Wanafunzi kupunguza msongomano madarasani pamoja na kusoma kwa urahisizaidi.

Aidha ameipongeza kampuni ya ujenzi wa Skuli hiyo kwa juhudi waliyoichukua kukamilisha majengo hayo pamoja na mshauri elekezi kwa  kuhakikisha ujenzi wa Skuli hiyo unamalizika kwa kiwango walichokubaliana.

Nae Mkurugenzi Idara ya Mipango Sera na Utafiti Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar bwana Khalid Salum Waziri amesema wameridhishwa na hatua waliyofikia ya ujenzi huo na kukubali kusaini fomu za makabidhiano ingawa kuna masuala madogo madogo ambayo yanahitaji kurekebishwa kwa haraka.

Amesema makabidhiano ya Skuli hiyo yanahusisha jengo la utawala na madarasa, mkahawa, mabweni ya wanawake, pamoja na nyumba za walimu nane, ambapo ujenzi wa mabweni ya wanaume bado yapo katika hatua za mwisho kukamilika.

Nae Mhandisi wa Ujenzi kutoka kampuni ujenzi huo RANS, bwana Yunus Ali Gare ameiahidi Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar kufanya marekesho yote ndani ya Wiki moja ili kuyaweka majengo yote katika hali ya ubora zaidi.

Aidha ameishukuru Wizara ya Elimu kwa kuwaamini na kuwapa tenda katika ujenzi huo na ameahidi kutoa ushirikiano katika kipindi chote cha majaribio ndani ya mwaka mmoja baada ya kukaidhiana.

Mapema mshauri elekezi wa ujenzi huo bwana Ali Juma Ali,
amesifu juhudi zilizochukuliwa na Mkandarasi wa Ujenzi wa Skuli hivyo na Kuisauri Wizara kulikubali jengo hilo kwa kasoro zilizojitokeza zinaweza kufanyika bila ya kuwepo kikwazo chohote.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.