Habari za Punde

Tatizo la Kizunguzungu linavyoisumbua jamii

 

LIJUWE TATIZO LA KIZUNGUZUNGU (DIZZINESS)  LINAVYOISUMBUWA JAMII

 

Takribani  kila mwaka watu milioni 8 huonana  na  wahudumu wa afya  kama madaktari  na wanasaikolojia wao  kutokana na kizunguzungu kisichoelezeka.

Tatizo la kizunguzuzungu  ni miongoni mwa matatizo sugu yanyowakumba watu wengi  katika jamii, kimsingi  tatizo hili  mara nyingi huwa ni  ishara ya tahadhari inayotolewa na mwili kuwa kuna kitu fulani hakiko katika hali ya  usawa, hivyo uchunguzi wa chanzo cha tatizo unapaswa kufanywa haraka. vile inavyowezekana.

NINI MAANA YA KIZUNGUZUNGU?

Kizunguzungu ni tatizo ambalo linaweza kumpata mtu yeyote na kuweza kupoteza utambuzi na uimara wa kiwiliwili chake. Kwa maana hiyo basi kizungu ni tatizo la haraka/ghafla linalotokana  ukosefu  wa kiasisi kidogo cha oksijini kwenye  ubongo/akili  na kuweza kushindwa kuhimili mizigo wa mwili husika na kuwa na udhaifu katika mwili,kichwa kuanza  na stim za mihemko,koptea kwa usawa wa mwili  na moyo kupiga pole pole.

SABABU ZA KIZUNGUZUNGU

Kizunguzungu si ugonjwa bali ni dalili  ya ugonjwa .Ziko sababu nyingi sana zinazompelekea mtu kupata/kusikia kizunguzungu katika maisha haya ya kila siku, nazo ni:

Ukosefu wa damu mwilini,au kupunguwa kwa mwendo kasi wa damu .Hali hii mara nyingi huwa  wanapata sana wanawake  pale ambapo wapo kwenye siku zao au wakati wa uja uzito hasa katika ile miezi mitatu ya mwanzo,kupungikiwa kwa sukar mwilini,Ugonjwa wa presha,kukosekana kwa  wa usingizi wa kawaida (insomnia),kuwa na msongo wa mawazo,maumivu ya kichwa,kuwa mja mzito hasa katika miezi mitatu ya mwazo,kwa baadhi ya wanawake kuwa kwenye mzunguko wao wa mwezi  kwani wengi huwa wanapoteza damu nyingi ,kumwa na unyusi baadhi ya magonjwa ya sikio kama vile uvimbe ndani ya sikio.ugonjwa wa mishipa ya fahamu,kuwa kwenye hali ya mfadhaiko,kufa ganzi mwilini,kupata na muangaza wa juwa kwa muda mrefu sana , kupungikiwa na maji mwilini.uvimbe kwenye ubongo kunakosababishwa na maumivu makali ya kichwa,ugonjwa wa kifafa ambao huambata na kupoteza ufahamu.ubigaji wa mastabesheni/ponyeto unaweza kupelekea kupata kizunguzungu,kuna baadhi ya tafiti zimeonyesha watu wamelala kwa muda mrefu kitandani kuna uwezekano mkubwa wa kupata kizunguzungu,na baadhi ya matumizi ya  dawa za kemikali au miti shamba bila mpangilio maalumu.

DALILI NA ISHARA ZA KIZUNGUZUNGU

 Mtu mwenye kizunguzungu  hujisikia kama kichwa chake kinazunguka zunguka,,kuyumba yumba, kujisikia mwepesi,kupunguwa nuru ya macho kwa ghafla,maumivu mepesi ya kichwa kizima,kujisikia/kuhisi umepungikiwa na pumzi mwilini,kuhisi marue rue,kuhisi kama unataka kuanguka,kupungukiwa kwa nguvu za kuona,kujisikia mnyovu mnyovu,kusikia kichefu chefu ,kama unatakutapika

MATIBABU YA KIZUNGUZUNGU

 Tatizo la kizunguzungu linaweza kudhibitiwa  kutoka  na utambuzi wa kile kilichosababisha  kizunguzungu

Ø  Hatua ya mwanzo unatakiwa ukae kitako na kufumba macho ikibidi  hata kulala chini

Ø  Kizunguzungu kinachotokana na upungufu wa damu mwilini mara nyingi hali husababisha  mwili kukosa hewa ya oksijeni ya kutosha. Kwa maana hiyo mgonjwa anatakiwa atumie vidonge vyenye madini ya chuma na ulaji wa mboga za kijani, maziwa, siagi na jibini husaidia kuondoa tatizo la kizunguzungu

Ø  kizunguzungu  kinachotokana  kuwa na msongo wa mawazo dawa pekee ni kujipumzisha na kuacha kuwaza kwa muda.ikiambatana na kufanya mazoezi mepesi mepesi ya kuvuta na kushusha pumzi

Ø  Kunywa maji kwa wingi hasa kwamba kizungunguzungu kimesababishwa na ukosefu wa maij mwilin  alau lita moja na nusu ilikurejesha virutubisho vilivyopotea kutokana na joto kali.

Ø  Kizunguzungu kilichosababishwa na ukosefu wa usinginzi, kinahitaji kushugulikiwa na mtaalamu wa masuala ya usingizi au kutibiwa hospitali, ni vizuri kuwasiliana na daktari mara moja kuhusu tatizo hilo.

Ø  Upungufu wa damu mwilini (Anaemia), nao husababisha kizunguzungu wakati mwingine, hali hii hutokana na mwili kukosa hewa ya oksijeni ya kutosha. Kula vidonge vyenye madini ya chuma na ulaji wa mboga za kijani, maziwa, siagi na jibini husaidia kuondoa tatizo la kizunguzungu.

Ø  Mwisho  kabisa  kwa vyoyote ikiwa kizunguzungu kitazidi kuendellea kila uchao  unatakiwa kuwaona timu ya madakitari  kama vile,daktari wa kiwiwili,daktari wa magonjwa ya akili, na mabingwa wa ushauri nasaha..

INDHARI

Itambulike kwamba sio kawaida  kwa mtu  mwenye  afya nzuri  kuweza kusikia kizunguzungu kila mara, kwa maana  hiyo  basi kama utajihisi unasumbuliwa na tatizo la kizunguzungu kila wakati ujue una tatizo ambalo unashauriwa kulifikisha katika hospital kwa uchunguzi zaidi.

USHAURI

Kwa kawaida, tatizo la kizunguzungu unaweza kulidhibiti mwenyewe kwa kutumia tiba mbadala ya kutengeneza mwenyewe nyumbani na kama tatizo litakuwa sugu, basi unashauriwa kumuona daktari mapema zaidi kabla hali hajawa mbaya zaidi.Vile vile  ni jambo zuri sana kwa kila mtu kujenga tabia ya kupima afya yake kila inapobidi pamoja na kuchunguza mwenendo wa mwili na kuchukua hatua za haraka za kudhibiti dalili zisizo za kawaida mwilini ili kujiepusha na maradhi hatari yanayoweza kuhatarisha maisha ya binadamu..

Imetayarishwa na:

Mohammed Sharksy

Mkufunzi Msaidizi,

Skuli ya Afya Sayansi za Tiba,

Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar, SUZA

0777432493 au email: mohammed.rashid96@yahoo.com,

ruruma96@gmail.com

 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.