Habari za Punde

UWT wafanya usafi katika Hoteli ya Paradaise Amani

Na  Takdir Suweid 

Mkoa wa Mjini Magharibi.                                                   11-01-2021.

 

Naibu Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mgeni Hassan Juma   amewataka Wakurugenzi wa Mabaraza ya Miji,Manispaa Miji na Halmashauri kuchukuwa hatua kwa Wawekezaji wanofanya Uchafuzi wa Mazingira katika maeneo yao.

 

Akishiriki katika zoezi la usafi huko pembezoni Mwa Hoteli ya Paradaise Amani Wilaya ya Mjini ikiwa ni Shamra Shamra ya kutimiza miaka hamsini na saba ya Mapinduzi ya Zanzibar ameagiza kuchukuliwa hatua za kisheria Wawekezaji watakaoshindwa kufanya usafi katika maeneo yao.


Amesema uharibifu wa Mazingira unapelekea kukwamisha Azma ya Serikali kufikia Uchumi wa Buluu na kuwataka Viongozi wa Mitaa kuripoti sehemu husika wakati wanapobaini mazingira machafu.

 

Aidha amewaomba Viongozi wa Shehia na Wadi kuweka Mikakati ambayo itaweka Mazingira kuwa Safi na kivutio kwa Wageni wanaoingia nchini.

 

Kwa upande wake Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mjini Fakharia Shomari Khamis  amesema akinamama wa UWT  Mkoa wa Mijini wamehamasika kuunga  Mkono Serikali katika kusafisha Mazingira ili Uchumi wa Buluu uendane na Usafi wa Mji.

 

Hata hivyo ametoa wito kwa Uongozi wa Baraza la Manispaa Mjini kufanya ziara za mara kwa mara katika maeneo mbalimbali ili kubaini waharibifu wa mazingira na kuwafikisha katika vyombo vya Sheria sambamba na kuwataka Wanachi kushirikiana na Serikali katika kufanya usafi.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.