BAADHI ya watu wenye ulamavu kutoka Jimbo la Gando
wakiwa na wazazi na ndugu zao, wakifuatilia kwa makini nasaha za Mbunge wa
Jimbo la Gando Salimu Mussa Omar, kabla ya kukabidhi vigari vya magurudumu
matatu kwa ajili ya walemavu.(PICHA NA
ABDI SULEIMAN, PEMBA)
BAADHI ya vigari vya magurudumu matatu ambavyo vipo
vinavyotumia umeme na visivyotumia umeme, vikikabidhiwa kwa watu wenye ulemavu
ndani ya jimbo la gando Wilaya ya Wete.(PICHA
NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)
MBUNGE wa Jimbo la Gando Kisiwani Pemba Salim Mussa
Omar, akizungumza na wananchi, wazazi, walezi na watu wenye ulemavu kabla ya
kukabidhi vigari vyenye magurudumu matatu hafla iliyofanyika hukpo Gando.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)
MBUNGE wa Jimbo la Gando Salim Mussa Omar, akimuweka
sawa katika kigari cha magurudumu matatu kijana Khamis Ali Nuhu ambaye
anaulemavu, baada ya kumkabidhi kigari hicho.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)
MBUNGE wa Jimbo la Gando Salim Mussa Omar,
akimuendesha kijana Salim Abdalla (Injinia) mwenye ulemavu wa miguu katika
kigari cha magurudumu matatu, baada ya kumkabidhi kigari hicho.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)
MBUNGE wa Jimbo la Gando Salim Mussa Omar,
akimuangalia kijana Salim Abdalla (Injinia) mwenye ulemavu wa miguu katika
kigari cha magurudumu matatu, akikiendesha kigari hicho baada ya kumkabidhi
kigari hicho.(PICHA NA ABDI SULEIMAN,
PEMBA)
No comments:
Post a Comment