Habari za Punde

Mkoa wa Tanga umetajwa kushika nafasi ya tano kwa kuwa na wazee wengi.


Na Hamida Kamchalla, TANGA.

KULINGANA na sensa ya watu na makazi iliyofanywa mwaka 2012 imeonesha kwamba mkoa wa Tanga una wazee wenye kuanzia miaka 60 wapatao 141,453 sawa na asilimia 6.9 na kuufanya kushika nafasi ya tano kati ya mikoa yote nchini.

Idadi hiyo ya wazee inachangiwa kwa kiasi kikubwa na idadi ku wa iliyopo wilayani Lushoto ambayo inaongoza kimkoa kwa kuwa na idadi ya wazee 36,575 kati ya wakazi 2,044,205 wakati wilaya ya Pangani ikiwa inashika nafasi ya mwisho kiwilaya kwa kuwa na wazee wapatao 4,167.

Ofisa ustawi wa jamii mkoani Tanga Mmassa Malugu alitoa takwimu hizo wakati akisoma maada ya utekelezaji wa masuala ya wazee kimkoa kwenye mkutano wa uzinduzi wa baraza la wazee mkoani hapa.

Malugu alisema kuwa kulingana na kuwepo kwa utaratibu wa mabaraza na taarifa kutolewa mara kwa mara wazee wameongezeka na kutambuliwa ambapo pia wapo ambao wamekwishasajiliwa na kupatiwa vitambulisho na kuongeza kuwa pamoja na kutambuliwa huko bado kuna tatizo sugu linalowakumba wazee kama vile kutoshirikishwa katika maamuzi yao.

"Mkoa wa Tanga tuna wazee wengi lakini sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012 imeonesha tuna asilimia 6.9 tu ya wazee, hii imekuja baada ya mkoa wa Pwani kuwa na asilimia 8.5, Lindi asilimi 9.0, Mtwara 9.5 wakati Kilimanjaro ikiongoza kwa asilimia 9.7 na kushika nafasi ya kwanza kwa kuwa na wazee wengi" alisema Malugu.

"Kutokana na taarifa kuhuishwa kila mwaka mkoa wetu mpaka kufikia mwaka jana tulikuwa na wazee wapatao 142,584 ambao wametambuliwa, na kati ya hao wazee 74,117 wamesajiliwa na kupatiwa vitambulisho vyao vya matibabu lakini zoezi hili linaendelea kwa kila halmashauri kulingana na bajeti zao" alifafanua.

Naye mkuu wa mkoa wa Tanga alitoa rai yake kwa wasajili kuwafikia wazee wote kwa ukaribu na kuwasajili ili wapate vitambulisho vitakavyowasaidia kupata huduma bure hospitali huku akiwasisitiza madaktari na wahudumu kuwapatia matibu kamili ikiwa ni vipimo pamoja na dawa ili kuwapunguzia garama badala ya kuwaandikia dawa za kununua.

Aidha Shigela aliwataka pia wanaotoa wanaochangisha pesa kwa ajili ya kuttoa huduma ya mifuko ya afya ya jamii kupeleka dawa hospitalini ili wananchi wanaochia wapate tiba nzuri zitakazowafanya kuendelea kuchangia mkfuko hiyo badala ya kukosa huduma wanapofika hospitalini na kuambiwa hakuna dawa.

"Nyie wasajili muwatafute wazee huko mitaani na vijijini muwasajili na muwape vitambulisho vyao vikawasaidie kufaidi huduma za matibabu, lakini pia mnaotoa huduma za mifuko ya afya ya jamii mjitahidi kule mahospotalini kuwe na dawa, siyo mnawachangisha wananchi pesa halafu bado wakifika wanaambiwa dawa ni za kununua, hii inakatisha tamaa mwishoni hawachangia tena" alisema.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.