STATE
HOUSE ZANZIBAR
OFFICE OF
THE PRESS SECRETARY
PRESS RELEASE
Zanzibar 18.02.2021

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi amemtumia salamu za rambirambi Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Joseph Magufuli kufuatia kifo cha Katibu
Mkuu Kiongozi Balozi John William Kijazi kilichotokea tarehe 17 Februari, 2021.
Balozi Kijazi
amefariki dunia majira ya saa 3:10 usiku akiwa katika Hospitali ya Benjamin
Mkapa, Jijini Dodoma alikokuwa akipata matibabu.
Salamu hizo za
rambirambi amezitoa kwa niaba ya wananchi wote wa Zanzibar na kueleza kwamba amepokea
kwa mshtuko na huzuni kubwa taarifa ya kifo cha Balozi John William Kijazi.
Salamu hizo zilieleza
kwamba yeye binafsi, familia yake pamoja na wananchi wa Zanzibar na wa Tanzania
kwa ujumla wamesikitishwa na kuhuzunishwa na kifo hicho.
“Namfahamu Balozi John William Kijazi
kuwa ni kiongozi mchapa kazi mahiri ambaye alikuwa na mashirikiiano mazuri na
wenziwe wote””, alieleza Rais Dk. Mwinyi katika salamu hizo za rambirambi.
Aidha, kupitia salamu hizo za rambirambi, Rais Dk. Mwinyi
alimuomba Mwenyezi Mungu kuwapa moyo wa subira na uvumilivu katika kipindi
hichi kigumu cha msiba, familia, ndugu pamoja na wananchi wote wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Rajab
Mkasaba, Ikulu Zanzibar
Postal Address: 2422 Tel.:0777427449. Fax:
024 2231822
E-mail: rajabmkasaba@yahoo.co.uk
No comments:
Post a Comment