Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk. Hussein Ali Mwinyi Atowa Mkono wa Pole kwa Familia ya Maalim Seif Nyali Mtambe leo.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk. Hussein Ali Mwinyi akitowa mkono wa pole kwa familia ya aliyekuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, nyumbani kwao kuifariji familia kabla ya kufanyika kwa mazishi katika Kijiji cha Nyali Mtambwe Wilaya ya Wete Pemba leo 18-2-2021 
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk. Hussein Ali Mwinyi akiitikia dua ikisomwa na Katibu wa Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Khalid Ali Mfaume (kushoto kwa Rais) wakati alipofika nyumbani kwa marehemu kutowa mkono wa pole kwa familia, kabla ya kuaza kwa mazishi ya aliyekuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad yaliofanyika Kijijini kwao Nyali Mtambwe Wilaya ya Wete Pemba na (kulia kwa Rais) Mkuu wa Wilaya ya Micheweni Pemba) CDR.Mohammed Mussa Seif na Katibu wa Rais Dkt. Abdalla Hasnu Makame.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.