Habari za Punde

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe Hemed Suleiman Abdulla Amtembelea Mjane wa Aliyekuwa Makamu wa Kwanza wa Rais Maalim Seif Sharif Nyumbani kwa Marehemu Mbweni.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman Abdulla akizungumza na Mjane wa aliyekuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Marehemu Maalim Seif Sharif Mama Aweina Sharif, alipofika kutowa mkuno wa pole kwa familia ya marehemu nyumbani kwao mbweni Jijini Zanzibar na mwenye baibui jeusi Mke wa Makamu wa Pili wa Rais Mama Sharifa Omar Khalfan. 
Mke wa Makamu wa Pili wa Rais Mama Sharifa Omar Khalfan akimfariji na kumpa pole mjane wa aliekuwa Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar Marehemu Maalim Seif Sharif Hamad katika makaazi yake Chukwani Zanzibar.

Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman Abdulla ameitembelea familia ya aliyekuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Marehemu Maalim Seif Sharif Hamad nyumbani kwao Mbweni Jijini Zanzibar kwa ajili ya kutowa pole na kuwafariji kufuatilia kwa msiba wa kuondokewa na mpendwa wao.

Makamu wa Pili wa Rais ameitaka familia hiyo kuwa na subra katika kipindi hiki pamoja nakuendeleza umoja na mshikamo aliouwacha marehemu Maalim Seif na serikali itaendelea kushirikiana na familia hiyo wakati wote.

Makamu wa Pili wa Rais alifutana na mkewe Mama Sharifa Omar Khalfan pamoja na viongozi wa wizara ya Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais sera, uratibu na baraza la wawkilishi.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.