RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akimsikiliza Bw. Munir Daya akitowa maelezo ya Kitabu cha Jumuiya hiyo kabla ya kumkabidhi, baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.na (kulia kwake) Mwenyekiti wa Jumuiya ya Khoja Shia Ithan Sheri Afrika kutoka Kampala Uganda Alhajj Shabir Najafi na Mamamu Mwenyekiti wa Bw. Aunali K.Khalfan a(Picha na Ikulu)
STATE
HOUSE ZANZIBAR
OFFICE OF
THE PRESS SECRETARY
PRESS RELEASE
Zanzibar
16.03.2021
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.
Hussein Ali Mwinyi ameikaribisha Jumuiya ya ‘Khoja Shia Ithna Ashir Jamaats of
African’ na kuitaka kuzitumia vyema fursa za uwekezaji na biashara zilizopo Zanzibar.
Dk. Miwnyi alieleza
hayo leo Ikulu Jijini Zanzibar wakati alipofanya mazungumzo na uongozi wa
Jumuiya ya ‘Khoja Shia Ithna Ashir
Jamaats of African’ ukiongozwa na Mwenyekiti wake Alhaj Shabir Najafi kutoka
Kampala Uganda.
Katika maelezo yake,
Rais Dk. Mwinyi alisema kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imefungua
milango yake katika sekta ya biashara na uwekezaji kwa ajili ya kukuza uchumi
na kuimarisha maendeleo hapa nchini.
Hivyo, Serikali
inawakabiribisha wawekezaji na wafanyabiashara wa Jumuiya hiyo kuzitumia fursa
hizo kwa kuja Zanzibar na kufanya shughuli za uwekezaji na biashara ili kuiunga
mkono Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika juhudi zake za kukuza uchumi na
kuwaletea wananchi maendeleo.
Rais Dk. Mwinyi
alisema kuwa kwa vile uchumi wa Zanzibar hivi sasa umejikita zaidi katika
uchumi wa buluu hivyo, ni vyema Jumuiya hiyo ikaangalia fursa zilizopo kupitia
uchumi huo ili iweze kuja kuekeza na kufanyabiashara hapa Zanzibar.
Aidha, Rais Dk. Mwinyi
aliueleza uongozi huo juhudi zinazochukuliwa na Serikali anayoiongoza katika
kuimarisha na kukuza uchumi wa Zanzibar.
Sambamba na hayo, Rais
Dk. Mwinyi aliipongeza Jumuiya hiyo kwa Juhudi zake za kuisaidia huduma za
Kijamii zikiwemo huduma za afya, maji, elimu na nyenginezo.
Rais Dk. Mwinyi
aliueleza uongozi huo kwamba bado wananchi wa Zanzibar wanahitaji huduma hizo
za kijamii hivyo ni vyema wakaitumia fursa hiyo kuwasaidia ikiwa ni kwa lengo
la kuiunga mkono Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kuwaletea maendeleo
endelevu wananchi wake.
Nae Mwenyekiti wa
Jumuiya hiyo Alhaj Shabir Najaf alimpongeza Rais Dk. Mwinyi kwa hatua yake ya
kuwakaribisha wawekezaji na wafanyabiashara kutoka Jumuiya hiyo kuja kufanya
shughuli zao hizo hapa Zanzibar.
Katika maelezo yake
Mwenyekiti huyo wa Jumuiya ya ‘Khoja Shia Ithna Ashir Jamaats of African’
aliahidi kulifanyia kazi suala hilo kwa kupitia Jumuiya yao pamoja na kuzitangaza
fursa zilizopo Zanzibar.
Mwenyekiti huyo pia,
alieleza utayari walionao wa kusaidia huduma mbali mbali za kijamii zikiwemo
huduma za maji, elimu, afya na nyenginezo.
Aidha, Alhaj Shabir
Najaf alimueleza Rais Dk. Mwinyi mikakati iliyowekwa na Jumuiya yao katika
kusaidia kutoa huduma za kijamii hapa Zanzibar.
Mapema Makamo
Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Aunali Khalfan ambaye ni mzaliwa wa Zanzibar kwa
niaba ya Jumuiya hiyo alimpongeza Rais Dk. Mwinyi kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi kwa kishindo.
Hivyo, walimuombea kwa
Mwenyezi Mungu kuendelea kumpa Rais Dk. Mwinyi afya njema pamoja na maisha
marefu ili aendelee kuiongoza Zanzibar na wananchi wake.
Sambamba na hayo,
Jumuiya hiyo ilitumia fursa hiyo kumpongeza Rais Dk. Mwinyi kwa kufanikiwa
kisiasa kutokana na hatua yake ya kuwaunganisha Wazanzibari na kuwafanya kuwa
kitu kimoja hali ambayo imepelekea kuwepo kwa amani, umoja na mshikamano hatua ambayo
itaipaisha Zanzibar kiuchumi na kimaendeleo.
Katika maelezo yake
Makamo Mwenyekiti huyo alieleza shughuli zinazofanywa na Jumuiya hiyo pamoja na
azma waliyonayo katika kuiunga mkono Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika
kuwasogezea wananchi huduma za kijamii zikiwemo maji, elimu, afya na nyenginezo.
Jumuiya hiyo iliyoanzishwa
mwaka 1946 na kusajiliwa hapa Tanzania mnamo mwaka 1960 kwa kupitia Jumuiya yake ndogo ya ‘Bilal Muslim Mission’
imeeleza azma yake ya kuisaidia Jamii kwa Unguja na Pemba katika kutoa
huduma zikiwemo za maji, afya, elimu
pamoja na kuwawezesha wanawake wajasiriamali hasa wale wa vijijini.
Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar
Postal Address: 2422 Tel.:0777427449. Fax:
024 2231822
E-mail: rajabmkasaba@yahoo.co.uk
No comments:
Post a Comment