Habari za Punde

Rais Dk Hussein Mwinyi awaapisha Mawaziri aliowateua karibuni

MAWAZIRI Wateule wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Kamishna wa Bodi ya Mapato Zanzibar ( ZRB) wakiwa katika ukumbi wa Ikulu Zanzibar wakisubiri kuapishwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) hafla hiyo ya kuapishwa imefanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar leo 4-3-2021.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akiwa amesimama wakati ukipigwa Wimbo wa Taifa kabla ya kuaza kwa hafla ya kuapishwa kwa Mawaziri na Kamishna wa ZRB katika ukumbi wa Ikulu  walioteuliwa hivi.(Picha na Ikulu)
VIONGOZI wa Serikali na Mawaziri Wateuli wakiwa wamesimama wakati ukipigwa wimbi wa Taifa na wa Afrika Mashariki kabla ya kuaza kwa hafla ya kuapisha, (kulia) Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman na (kushoto) Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman Abdulla, Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe. Omar Othman Makungu na Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Mhe. Dkt, Mwinyi Talib Haji.(Picha na Ikulu)


RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akimuapisha Dkt. Saada Mkuya Salum kuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais, hafla hiyo ya kuapishwa imefanyika leo 4-3-2021 katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akimuapisha Mhe. Nassor Ahmed Mazrui kuwa Waziri wa Afya,Ustawi wa Jamii,Wazee Jinsia na Watoto Zanzibar, hafla hiyo ya kuapishwa imefanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar leo 4-3-2021.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akimkabidhi hati ya kiapo Waziri wa Afya Ustawi wa Jamii, Wazee,Jinsia na Watoto Zanzibar Mhe. Nassor Ahmed Mazrui, baada ya kumaliza kula kiapo, hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akimuapisha Mhe. Omar Said Shaaban, kuwa Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Zanzibar, hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu)

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akimkabidhi hati ya kiapo Waziri wa Biashara na Maendelo ya Viwanda Zanzibar  Mhe. Omar Said Shaaban baada ya kumaliza kuapa, hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar leo 4-3-2021.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akimuapisha Ndg.Salum Yussuf Ali kuwa Kamishna wa Bodi ya Mapato Zanzibar (ZRB) hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akimkabidhi hati ya kiapo Kamishna wa Bodi ya Mapato Zanzibar(ZRB) Ndg. Salum Yussuf Ali, baada ya kumaliza kula kiapo, hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu)
WAKUU wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama Zanzibar na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe. Idrisa Mustafa Kitwana (kulia) wakifuatilia kuapishwa kwa Mawaziri na Kamishna wa ZRB, waliochaguliwa hivi karibuni hafla hiyo iliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu)
BAADHI ya Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar wakifuatilia kuapishwa kwa Mawaziri na Kamishna wa ZRB walioteuliwa hivi karibuni na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi.(hayupo pichani) hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akiwa katika picha ya pamoja na Mawaziri na Kamishna wa ZRB aliowaapisha katika ukumbi wa Ikulu. (kulia kwa Rais) Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais.Mhe.Dkt. Saada Mkuya Salum na Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Zanzibar Mhe.Omar Said Shaabn na (kushoto kwa Rais) Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla, Waziri wa Afya,Ustawi wa Jamii, Wazee,Jinsi na Watoto Zanzibar Mhe. Nassor Ahmed Mazrui na Kamishna wa Bodi ya Mapato Zanzibar (ZRB) Ndg. Salum Yussuf Ali.(Picha na Ikulu)


 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.