Habari za Punde

Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Samia Suluhu Hassan Akiwaongoza Wananchi wa Tanzania Katima Maziko ya Hayati Dkt.John Pombe Magufuli Kijijini Kwao Kilimani Chato Mkoano Geita leo.

Makamanda wa Jeshi la Wananchi la Tanzania JWTZ wakiwa wamebeba jeneza likiwa na Mwili wa Hayati Dkt.John Pombe Magufuli wakati wakiingia katika eneo la makaburi katika makazi ya marehemu Kilimani Mkoani Geita Chato. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Mama Janeth Magufuli Mjane wa  aliyekuwa Rais wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Hayati Dkt. John Pombe Magufuli wakati wa Mazishi yake yaliyofanyika leo March 26,2021 katika Makaburi ya Familia Kijijini kwake Chato Kilimani Mkoani Geita.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akilihutubia Taifa Mara Baada ya kumalizika Misa Maalum kwa ajili ya aliyekuwa Rais wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Hayati Dkt. John Pombe Magufuli iliyofanyika leo March 26,2021 katika Uwanja wa Magufuli Wilayani Chato wakati wa Maandalizi ya Mazishi yake yaliyofanyika katika Makaburi ya Familia Kijijini kwake Chato Kilimani Mkoani Geita.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akitia Udongo kwenye Kaburi wakati wa Mazishi ya aliyekuwa Rais wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Hayati Dkt. John Pombe Magufuli yaliyofanyika leo March 26,2021 katika Makaburi ya Familia Kijijini kwake Chato Kilimani Mkoani Geita.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiweka Shada la Maua kwenye Kaburi la aliyekuwa Rais wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Hayati Dkt. John Pombe Magufuli wakati wa Mazishi yake yaliyofanyika leo March 26,2021 katika Makaburi ya Familia Kijijini kwake Chato Kilimani Mkoani Geita.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.