Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi Amemteua Othman Masoud Othman.Kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar.

 

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi amemteua Othman Masoud Othman Sharif kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar.

Katika taarifa ya vyombo vya habari iliyotolewa na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena Ahmed Said ilieleza kwamba kwa kuzingatia matakwa ya Kifungu cha 9(3)cha Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984, kinachosema kwamba “Muundo wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar utakuwa wa Umoja wa Kitaifa na utendaji wa kazi zake utafanywa katika utaratibu utakaohakikisha kuendelezwa kwa umoja nchini na lengo la kufikia demokrasia”.

Hivyo, kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya Kifungu Namba 39(3) cha Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984, baada ya kushauriana na Chama cha ACT-Wazalendo, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi amemteua Othman Masoud Sharif kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar.

Uteuzi huo umeanza leo tarehe 01 Machi, 2021.

Sherehe ya kuapishwa kwa Makamu huyo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar itafanyika kesho tarehe 02 Machi, 2021 saa 4:00 asubuhi katika Ukumbi wa Ikulu, Zanzibar.

Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar

Postal Address: 2422 Tel.:0777427449. Fax: 024 2231822 

 E-mail: rajabmkasaba@yahoo.co.uk

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.