Habari za Punde

Makamu wa Pili wa Rais Mhe Hemed ajumuika na waumini kusali sala ya Ijumaa Masjid Rahman, Fuoni

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla akitikia maombi ya dua Maalum iliongozwa na Imamu mara baada ya kukamilika kwa sala ya Ijumaa iliosaliwa katika Masjid Rahman Fuoni.
Waumini wa Dini ya Kislamu wa Masjid Rahman Fuoni wakifuatilia kwa makini houtuba ya Sala ya Ijumaa iliotolewa na Khatibu aliohutubu Makitini hapo Al-Ustadhi Fakih Mohammed Ausi.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla akisalimiana na Waumini wa Dini ya Kislamu wa Masjid Rahman Fuoni mara baada ya kukamilika kwa Sala Ijumaa.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla akimsalimia moja ya mtoto aliefika kutekeleza Sala ya Ijumaa katika Masjid Rahman Fuoni.  


Na Kassim Abdi OMPR

Waumini wa Dini ya Kislamu wametakiwa kuzingatia vyema mafunzo waliyoyapata katika kipindi cha mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani ili kuendeleza mapenzi, huruma na uchamungu.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed  Suleiman Abdulla  alieleza hayo wakati akizungumza na waumini wa Masjid Rahman uliopo Fuoni mara baada ya kukamilika kwa ibada ya sala ya Ijumaa.

Alisema katika kuelekea kuisherehekea skukuu ya Eid Fitri amewaomba wazazi na walezi kuwachunga watoto wao kwa kuzingatia maadili na taratibu za dini ya kIslamu ili kuepuka kuchupa mipaka iliowekwa na Allah (S.W).

Katika kuelekea kusherekea Skukuu hiyo Makamu wa Pili wa Rais alitumia fursa hiyo kuwaeleza waumini na wanachi wa Zanzibar  kwa ujumla juu ya vitendo vya udhalilisha  kuwa kuna uwezekano wa kudhibitiwa kwa vitendo hivyo endapo kila mtu atatimiza wajibu wake.  

Mhe. Hemed aliwaomba viongozi wa dini kuendelea kuiombea dua nchi pamoja na viongozi wake ili wananchi wake wandelee kuwa wamoja jambo ambalo litasaidia kwa kiasi kikubwa kujenga mustkbali mwema wa Amani na Utulivu.

Nae Khatib alihutubu katika mskiti huo Al-Ustadhi Fakih Mohammed Ausi aliwakumbasha waumini baada ya kukamilika kwa funga ya Ramadhani hawana budi kuendeleza kufunga siku Sita za mwezi wa Shauwal kwani kuna malipo makubwa kutoka kwa M/Mungu kwa wafungaji wake.

Aidha, Al-Ustadhi Fakih katika houtuba yake alipongeza serikali ya Mapainduzi ya Zanzibar kwa hatua ya kupiga marufuku upigwaji wa Muziki katika viwanja vya skukuu kwani kufanya hivyo kumesaidia kwa kiasi kikubwa kuipa hadhi Skukuu inayosherekewa na Waislamu nchini kote.

Aliwakumbusha waumini na wananchi Nchini kuendelea kuuiunga mkono serikali yao kutokana na mambo mazuri yanayotekelezwa na viongozi kwani yanalenga kuimarisha uwajibikaji na kuweka sawa nidhamu za watumishi wake.

 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.