Habari za Punde

Wafanyakazi wa Ofisi ya Makamu wa Rais Wajumuika Katika Futari Maalum Walioandaliwa.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Selemani Jafo akiwaongoza watumishi wa Ofisi hiyo katika hafla ya futari kwa ajili ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani iliyofanyika jijini Dodoma.

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Bi. Mary Maganga akipakua futari wakati wa hafla iliyoandaliwa kwa ajili ya watumishi wa Ofisi hiyo ikiwa ni sehemu ya Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Selemani Jafo akizungumza na watumishi wa Ofisi hiyo wakati wa hafla ya futari iliyoandaliwa kwa ajili ya watumishi hao katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, iliyofanyika jijini Dodoma ambapo aliwaasa Watanzania kuliombea Taifa liendelee kuwa na Amani.

Pia aliwataka watumishi hao kuendelea kudumisha upendo na kuwasaidia wananchi wanawahudumia ambapo pia alitumia nafasi hiyo awatakia heri katika Mfungo Mtukufu wa Ramadhani kuelekea Sikukuu ya Eid.

Kiongozi wa dini ya Kiislamu akiomba Dua kwa ajili ya hafla ya futari iliyoandaliwa kwa ajili ya watumishi wa Ofisi ya Makamu wa Rais iliyofanyika jijini Dodoma Mei 11, 2021.
No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.