Habari za Punde

Abdul- Latif ashinda Urais ZFFNa Mwandishi Wetu

Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Soka la Zanzibar (ZFF) wamemchagua kwa Kura za Ndio, Ndug. Abdul-latif Ali Yassin kuwa Rais wa Shirikisho hilo baada ya Kupata kura 16 katika kura 24 za Wajumbe wote zilizopigwa.


Abdullatif ameshinda nafasi hiyo Baada ya Kupata Kura 16, Sawa na Asilimia 67% akimshinda Ndug. Suleiman Shabani Suleiman aliepata kura 8 sawa na Asilimia 33% kwa Hatua ya Pili ya Mchakato wa kupiga kura.


Awali Abdullatif alipata kura 11, Suleiman Mohammed Jabir alipata kura 6, Suleiman Shabani Suleiman alipata kura 7, huku Abdul-kadir Mohammed pamoja na Haji Sheha Hamad ambao hawakupata kura hata moja, Matokeo ambayo yalilazimisha kurudiwa kwa Zoezi la upigaji wa Kura kutokana na Mshindi wa Kura za Awali kutofikia Asilimia 50.1% ya kura zilizopigwa kama Katiba inavyoelekeza.


Kwa Matokeo hayo, Abdullatif Ali Yassin anakuwa Rais wa Shirikisho la Soka la Zanzibar (ZFF)


Zoezi la Upatikanaji wa Rais huyo limeshuhudiwa na Kaimu Waziri wa Habari, Vijana Utamaduni na Michezo ambae ni Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale, Mh: Leila Mohammed Mussa pamoja na Viongozi mbali mbali wa Wizara, Idara na Shirikisho la Mpira wa Miguu Zanzibar (ZFF)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.