Habari za Punde

Bei mpya za mafuta zitakazoanza kesho

 Mwashungi Tahir   Maelezo                        8-6-2021.

Mamlaka ya Udhibiti wqa Huduma za Maji na Nishati Zanzibar  (ZURA) imefanya mabadiliko ya bei za mafuta  zitakazoanza kutumika rasmi kuanzia siku ya Jumatano Tarehe 09-06-2021.

Akizungumza na waandishi wa habari huko Ofisini kwake Maisara Afisa wa Uhusiano Mbaraka  Hassan Haji wakati alipokuwa akitoa taarifa kwa umma juu ya mabadiliko ya bei za mafuta inayotarajiwa kuanza kesho.

Amesema ZURA inapanga bei kwa kuzingatia mambo matano  ambayo ni wastani wa mwenendo wa mabadiliko ya bei za mafuta Duniani (Platts Quatations) katika mwezi wa Mei 2021, kwa lengo la kupata kianzio cha kufanya mabadiliko ya bei  za mafuta Juni 2021.

Pia mambo mengine ni gharama za uingizaji katika Bandari ya Dar es salaam , thamani ya shilingi ya Tanzania kwa Dola, gharama za usafiri, Bima na ‘Premium ‘ hadi Zanzibar, kodi za Serikali na kiwango cha faida kwa wauzaji kwa jumla na Rejareja.

Aidha amesema Mafuta ya Petroli katika mwezi wa Mei 2021bei (TZS/LITA) 2,195  bei ya mwezi wa Juni itakuwa (TZS/LITA)2,272 TOFAUTI (TZS)77sawa na asilimia 3.51.

Mafuta ya Dizeli  katika mwezi wa Mei , 2021 bei (TZS/LITA)2,148 bei ya mwezi Juni itakuwa (TZS/LITA)2,182 Tofauti (TZS)34 sawa na asilimia 1.58.

Kwa upande wa Mafuta ya Taa  katika Mwezi wa Mei 2021 bei (TZS/LITA)1,546 BEI YA MWEZI WA Juni itakuwa (TZS/LITA)1,546 Tofauti  0 sawa na asilimia 0.00

Mbaraka amesema bei ya mafuta Petroli , Dizeli na Mafuta ya Taa zimeongezeka katika Mwezi wa Juni, 2021 ikilinganuishwa na Mwezi wa Mei , 2021 kutokana na kubadilika kwa wastani wa bei za uuzaji wa bidhaa hizo katika soko la dunia pamoja na soko la ndani kwa kupitia bandari ya Dae es salaam.

Ameeleza kwamba ZURA uinapenda kuwajuilisha wananchi kuwa bei hizo ndio bei halali zinazotangazwa na kutumika kuanzia kesho  na kuwanasihi kununua bidhaa hizo katika vituo  na baada ya kununua wadai risiti.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.