Habari za Punde

Majiliwa atoa Maagizo kwa Wizara, Wakuu wa Mikoa na Wilaya.

Na. Mwandishi Wetu-MAELEZO

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa, amesema kuwa Serikali inafanya kazi kwa kushirikiana na Sekta binafsi katika kuboresha mazingira ya biashara kwani imejipanga kuondo changamoto ili kuwezesha wafanyabiashara na wawekezaji wanainua mitaji yao.

Akizugumza katika Mkutano wa Baraza la Biashara la Taifa (TNBC) na Siku 100 za Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu alisema kuwa Serikali itahakikisha kila changamoto zote ambazo zipo katika maeneo mbalimbali nchini ambazo zinaweza kukwamisha ukuaji wa biashara na uwekezaji Serikali itazitaua na amewaagiza Wakuu wa Mikoa, Wilaya na Wizara ambazo kutekeleza maagizo ya Mhe. Samia Suluhu Hassan ya kuboresha mazingira ya biashara

“Serikali inayongozwa na Mhe. Samia Suluhu Hassa, iko pamoja nanyi sekta binafsi, jukumu letu ni kuhakikisha kuwa mnapata mafanikio makubwa pale mlipowekeza, lakini pia tutahakikisha kuwa tunashirikiana nanyi ili kuwezesha utatuzi wa changamoto mbalimbali na tutahakikisha huduma zote zikiwemo maji, umeme, barabara na ardhi kwa ajili ya wafanyabishara na wawekezaji zinapatikana bila urasmu”, Alisema Kassim Majliwa

Aidha, Waziri Mkuu alitoa maagizo wa Wizara, Wakuu wa Mikoa na Wilaya pamoja na Taasisi ambazo zimeguswa na Maadhimio ya Mkutano wa 12 wa Baraza la Biashara kuhakikisha kuwa zinatekeleza maagizo hayo ili kutatua changamoto kwa wawekezaji.

Akibainisha maagizo hayo, Mhe. Majaliwa amesema kuwa Wakuu wa Mikoa na Wilaya wahakikishe wanaunda mabaraza ya biashara na kama mabaraza hayo tayari yapo wahakikishe kuwa yanakutana mara kwa mara ili kuweza kusaidia utekelezaji wa kuboresha biashara kuanzia ngazi za chini kwenye halmashauri.

“Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya kote nchini undeni mabaraza ya biashara ili kurahisha muunganyiko wa majukumu ya wafanyabiashara na Serikali, lakini pia kama mabaraza haya yapo yahakikishe yanakutana na kufanya mazungumzo na sekta binafsi ili kuinua biashara na kukuza mitaji ya wafanyabiashara”, alisistiza Mhe. Kassim Majaliwa.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu aliiagiza Wiazara ya Viwanda, Taasisi ya Misitu nchini kukutana  sekta binafsi, Wadau wa mazao ya misitu pamoja na wafanyabiashara na wamiliki wa viwanda vya mbao ili kuzungumza jinsi ya kuinua biashara ya mazao ya misitu ikwemo mbao.

Waziri Mkuu, aliongeza kuwa Taasisi za umma ziendelee kutoa huduma kwa weledi kwa wafanyabiashara na wawekezaji ili waondokane na changamoto na aliahidi kuwa Serikali itandelea kutoa huduma bora ya maji, barabara, umeme na ardhi.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.