WATENDAJI kutoka tume
ya Kitaifa ya kuratibu na udhibiti wa Dawa za kulevya Pemba, pamoja na vijana
walioacha kutumia dawa kulevya kutoka Soba House ya Mkoroshoni, wakifanya usafi
katika Hospitali ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba, ikiwa ni shamrashamra za
maadhimisho ya siku ya kupiga vita Matumizi na Usafirishaji wa dawa za kulevya
Zanzibar, shamrashamra hizo Pemba zimeanza Juni 20 mwaka huu
WANAFUNZI kutoka Chuo cha Afya Pemba, wakifuatilia kwa makini mafunzo ya siku juu ya athari za matumizi ya dawa za kulevya kwa jina, ikiwa ni shamrashamra za maadhimisho ya siku ya kupiga vita Matumizi na Usafirishaji wa dawa za kulevya Zanzibar, shamrashamra hizo Pemba zimeanza Juni 20 mwaka huu.
(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)
No comments:
Post a Comment