Habari za Punde

Mhe Masoud: Zanzibar inahitaji uongozi wenye uoni na dhamira ya kweli ili kuikuza nchi

Mjumbe wa Kamati Kuu wa chama cha ACT wazalendo ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar Othman Masoud Othman akivishwa koja na Bimize Kombo Hamad mara alipowasili Wilaya ya Micheweni katika ziara iliyoandaliwa na chama hicho kwa ajili ya kumtambulisha kwa viopngozi wa Mikoa Majimbo na Matawi.
Katibu wa Ngome ya wanawake  Chama cha ACT wazalendo Jimbo la Wingwi  Biache Othman Ramadhan akimkabidhi zawa aina ya Kuku Mjumbe wa Kamati Kuu wa chama hicho ambaye ni Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar Othman Masoud Othman alipofika katika mkumbi wa halimashauri  Wilaya ya Micheweni katika ziara iliyoandaliwa ya kumtambulisha kwa viongozi wa Mikoa, Majimbo na Matawi.

Na Talib Ussi. Pemba.

Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha ACT wazalendo amesema Zanzibar inahitajika uwongozi wenye uoni na dhamira ya kweli ili kuikuza nchi kiuchumi.

Aliyaeleza hayo huko Wilaya ya  Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba katika Ukumbi wa Halmashauri akiwa katika ziara iliyoandaliwa na chama hicho kwa ajili ya kumtambulisha kwa viongozi wa Mikoa, Majimbo na Matawi.

Mhe.Othman ambaye pia ni Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar ameitaja Serikali ya Umoja wa kitaifa (JNU) na Viongozi wake kuwa hatua muhimu ya kuelekea matarajio hayo.

Alieleza kuwa mataifa mengi Duniani yameweza kuendelea kutokana na uoni wa viongozi wake na kutolea mfano nchi ya Singapore na kueleza kuwa wasingeweza kuendelea bila ya uwepo wa uoni wa viongozi wao.

Alieleza kuwa Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr Husein ili Mwinyi  ameonyesha uoni wa kuinyanyua Zanzibar kiuchumi.

“Lakini kama atakuwa Rais pekee na wengine wakakosa uoni wa maendeleo basi tunaweza kumuumiza kifua na kuwa ngumu” alisema Othman.

Alisema kuwa Rais wa Zanzibar amekuwa akishishitiza maridhiano kwa sababu uoni wake unamuanyesha ili Zanzibar ipaae juu kiuchumi lazima uwepo umoja wa kitaifa

Alisema ni lazima kila mmoja awe na uoni wa kuirudisha Zanzibar katika hatua ambayo ilifikia kiuchumi mnamo miaka ya 1960.

Alieleza kuwa Zanzibar ilikuwa nchi ya tatu barani Afrika kiuchumi lakini leo imeshuka.

“Tumekuwa tukimsikia Rais wetu akiwatumbua wabadhirifu kwa sababu uoni wake umeona wanamkwamisha katika juhudi zake za kuinyanyua Zanzibar kiuchumi”  alisema Othman.

Sambamba na hilo alisema fikra hiyo itaweza kufikiwa ikiwa kila kiongozi atakuwa Muwadilifu katika kutekeleza majukumu yake.

Alieleza kuwa kama viongozi watakuwa wanakwenda kinyume na maadili ya utumishi wa umma itakuwa kikwanzo kikubwa kuwa na vbiongozi wenye uoni wa kuinyanyua Zanzibar kiuchumi.

Alisema tayari Rais ameshawasimamisha viongozi wengi ambao sio wadilifu katika nafasi ambazo wamepewa.

Mapema akimkaribisha kiongozi huyo wa Pili katika safu ya uongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) Makamu mwenyekiti wa chama cha Act wazalendo Zanzibar Juma Duni Haji alisema imefika muda kwa masheha wa Zanzibar kufuta lawama ambazo hupokea kutoka kwa wananchi kutokana kuwanyima vitambulisho vya Mzanzibari (Mkaazi Zan ID).

Alisema kwa sababu Waziri husika amesema hadharani kuwa sheha yeyote atakaye mnyima mwananchi kitambulisho hicho atachukuliwa hatua na kuhoji kwa nini Sheha akubali kuadhirishwa.

“Hemu Masheha ogopeni na wacheni lawama ambazo hazina faida kwako, wala familia yako” alisema Duni Maarufu Babu Juma.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.