Mkurugenzi Kinga na Elimu ya Afya Zanzibar Dkt. Fadhil Mohamed Abdalla akifungua mafunzo ya Uhamasishaji Chanjo ya Kipindupindu kwa wandishi wa Habari chanjo itayoanza kutolewa tarehe 3 mpaka 7 mwezi wa saba 2021 na awamu ya pili tarehe 31 mpaka 4 mwezi wa 8, mafunzo yaliyofanyika ukumbi wa mikutano Wizara ya Afya Mnazimmoja Mjini Zanzibar.
Mkuu wa Kitengo cha Elimu ya Afya Halima Ali Khamis akiwasilisha mada ya uhamasishaji Chanjo ya Kipindupindu kwa wandishi wa Habari katika ukumbi wa mikutano Wizara ya Afya.
Baadhi ya wandishi wa Habari wakifuatilia mafuzo kuhusu Chanjo ya Kipindupindu kwa Mkuu wa Kitengo cha Elimu ya Afya Halima Ali Khamis (hayupo pichani) alipokuwa akitoa mada yake
Afisa kutoka (WHO) Dkt. Vendelin Simon akijibu maswali ya wandishi wa habari (hawapo pichani) katika Mafunzo ya Chanjo ya Kipindupindu yaliyofanyia ukumbi wa mikutano Wizara ya Afya.
Picha na Makame Mshenga.
No comments:
Post a Comment