Habari za Punde

MNEC Masoud - Amnadi Mgombea Ubunge wa CCM Jimbo la Konde Pemba Katika Kampeni za Uchaguzi Mdogo.

 Na.Is-Haka Omar - PEMBA.

MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (TAIFA) Taifa Masoud Ali Mohammed, amewahakikishia wananchi wa Jimbo la Konde kwamba Chama hicho kitaendelea kuheshimu makubaliano ya mkataba wa kuwatumikia wananchi ambao ulifungwa mwezi Oktoba mwaka 2020.

 

Aidha amesema utekelezaji wa mktaba huo utaendelea kuimarishwa zaidi kwani lengo la CCM ni kuwatumikia  wananchi wa makundi yote bila upaguzi wa kiitikadi,kidini,kirangi na kikabila.

 

Masoudi aliwambia wananchi hao kwamba, kipaumbe kikubwa cha CCM ni kuhakikicha wananchi wanapata kwa wakati huduma zote za kijamii,kiuchumi sambamba na kuimarisha sera zake za misiasa ziendane na matakwa ya jamii husika.

 

Hayo ameyasema wakati akizungumza na wananchi wa Jimbo la Konde kwenye mkutano wa Kampeni za uchaguzi mdogo jimbo hilo  uliofanyika kwenye viwanja vya Msuka.

 

Masoud ambaye pia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa, na Idara Maalumu za SMZ  amewataka wananchi hususani wapiga kura kufanya maamuzi sahihi ya kuchagua mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM Sheha Mpemba Faki ikikapo Julai 18 mwaka 2021ili aendelee kutekeleza Ilani ya CCM kwa lengo la kuwaletea maendeleo endelevu ndani ya Jimbo hilo.

 

“ Chama Cha Mapinduzi kimemsimamisha Ndugu yetu Shaha Mpemba Faki kugombea nafasi ya Ubunge hivyo nakuombeni mfanye maamui sahihi kwani mgombea huyu ana sifa zote za kuwatumia wananchi na pia anafahamu vizuri Jimbo la Konde”, alisema Massoud.

 

Mapema Mwakilishi wa Jimbo la Konde Zawadi Amour Nassoro, amewasihi wapiga kura kumchagua mgombea huyo wa tiketi ya CCM  ili washirikiane katika kuimarisha maendeleo ya jimbo hilo sambamba na kuanzisha miradi mipya ya kiuchumi itakayowasaidia wananchi wa jimbo hilo kujikwamua kimaendeleo.

 

Naye Mbunge viti Maalumu wanawake Mkoa wa Kaskazini Pemba Asiya Sharrif Omar, amesema  kwamba Ilani ya uchaguzi ya  Chama Cha Mapinduzi imetekelezwa kwa asilimia kubwa katika Jimbo hilo, hivyo panahitajika kiongozo mwenye maono na nia ya dhati ya kuwatumikia wananchi anayetokana na CCM ili alinde na kuendeleza maendeleo ya jimbo la konde.

 

Katika ahadi yake kwa wananchi baada ya kukabidhiwa Ilani ya Uchaguzi, Mgombea Ubunge wa Jimbo hilo Sheha Mpemba Faki alisema endapo akipewa nafasi hiyo atahakikisha anaanisha vikundi vya ujasiriamali kwa Vijana na akina Mama pamoja na kutoa motisha kwa wanafunzi wa kidato cha nne ambao watapata daraja la kwanza kwenye mitihani yao ya Taifa.

 

Katika maelezo yake mgombea huyo aliahidi kutekeleza Ilani ya CCM ya mwaka 2020/2025 kwa kasi ili kuhakikisha anatatua changamoto zinazowakabili wananchi wa jimbo hilo kwa muda mrefu.


"Nakuombeni Wananchi wenzangu wa Jimbo la Konde mniamini na kuridhia kunichagua kwa kura nyingi, naahidi kukutumikieni kwa uadilifu,uzalendo na wema bila ubaguzi kwa kuhakikisha jamii yote ya jimbo letu inanufaika na fursa mbalimbali zitakazopatikana zitakuwa ni kwa ajili ya Wana Konde", aliomba ridhaa ya kuchaguliwa Sheha Mpemba.


Akizungumza kwenye mkutano huo, Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya CCM Mkoa wa Kaskazini Pemba ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa  huo Salama Mbarouk Khatib, amewataka wananchi wenye sifa kujitokeza kwa wingi katika vituoni vya kupiga kura na kwamba hali ya ulinzi itaimarishwa.

 

Uchaguzi Mdogo Jimbo la Konde utafanyika julai 18 mwaka huu na unafanyika baada ya kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo kupitia chama cha ACT Wazalendo Marehemu Khatib Said Haji kilichotokea miezi miwili iliyopita.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.