Habari za Punde

Uongozi wa Chuo Cha Amali Daya Mtambwe Kufanya Kazi Kwa Bidii.-Mhe.Simai.

Na Ali Suleiman, WEMA PEMBA.

Waziri wa Elimu na Maafunzo ya Amali Mhe. Simai Mohammed Said ameutaka uongozi wa Chuo cha Mafunzo ya Amali Daya Mtambwe kufanya kazi kwa bidii itakayopelekea mafanikio kwa Wanafunzi wa mkupuo wa kwanza.

Mhe. Simai ameyasema hayo Wakati akizungumza na uongozi wa Chuo cha Amali Daya Mtambwe Wakati alipofanya ziara kukitembelea Chuo hicho na kujionea shughuli mbali mbali za Masomo zinazoendelea katika Chuo hicho.

Akizungumza na Wafanyakazi Mhe. Simai  amewataka watendaji hao kukabiliana na changamoto ya iliopo juu ya uhaba wa Wafanyakazi hao kwa kufanya kazi kwa bidii ili mafanikio yaweze kupatikana kupitia Wanafunzi wa mkupuo wa awali.

Amesema moja kati ya fani zinazotolewa katika Chuo hicho ni fani ya Uvuvi ambayo inalenga kuwaandaa vijana kuweza kufikia Malengo ya Serikali ya Awamu ya nane kuelekea Uchumi wa buluu.

Mhe, Simai ameelezea matumaini yake kuwa bwawa linalotarajiwa kujengwa kwa ajili ya mafunzo ya vitendo vya fani  ya Uvuvi, litatoa fursa na kwa  wanajamii kujifunza kuogelea katika bwawa hilo ili kuongeza nafasi zaidi katika fani hiyo.

Aidha ameutaka uongozi, wafanyakazi na Wanafunzi wa Chuo hicho kutilia maanani suala la utunzaji wa mazingira kwa kupanda bustani na miti mbali mbali Ili kuboresha mandhari ya Chuo hicho.

Kwaupande wake Afisa Mdhamini Wizara ya Elimu na Maafunzo ya Amali mwalimu Moh'd Nassor Salim amewataka Wanafunzi kuitumia vyema fursa waliyoipata kwa kuweka historia sio tu ya kua Wanafunzi wa mwanzo bali pia waweze kufaulu vizuri masomo yao.

Nae Kaimu Mratibu Mamlaka ya Mafunzo ya Amali Ndugu Othman Zaid Othman amesema Chuo kimeshafanya usajili kwa Wanafunzi wa mkumbo wa mwanzo ambapo jumla ya wanafunzi 175 wamesajiliwa na kuanza Masomo yao katika fani mbali mbali.

Ndugu Othman ametaja baadhi ya fani hizo pamoja na kilimo,  umeme, ufundi magari, useremala na mapokezi  ambapo jumla ya wanafunzi 25 wameeomba huku fani ya Uvuvi ikiwa na jumla ya Wanafunzi 50.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.