Habari za Punde

Vitendo Vya Udhalilishaji Vimeonekana Kuongeza Katika Mwezi.

Na  Mwashungi  Tahir    Maelezo    16-7-2021.

Vitendo vya ukatili na udhalilishaji wa kijinsia  kwa watoto vimeonekana kuongezeka kwa Mwezi huu na kuwepo  idadi kubwa ya vitendo hivyo hali ambayo inapelekea kuharibu  mustakbali mzima malengo yaliyokusudiwa na jamii .

Akizungumza na waandisha  habari katika uwasilishaji wa Takwimu za Ukatili na Udhalilishaji wa Kijinsia kwa Wanawake na Watoto  Mtakwimu Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali katika kitengo cha Makosa ya Jinai, Madai na Jinsia Ramla Hassan Pandu huko katika ukumbi wa Mtakwimu Mkuu wa Serikali uliopo Mazizini

 

Amesema kuwa  jumla ya matukio  97 ya ukatili na udhalilishaji wa kijinsia yameripotiwa Mwezi wa Juni mwaka huu  ukilinganisha na Mwezi uliopita yameongezeka 66 kwa mwezi wa Mei2021.

 

Ameeleza kuwa Wilaya ya Magharibi 'A' inaongoza kuwa na idadi kubwa ya matukio hayo ambapo yalikuwa matukio 25 ukifuatiwa na wilaya ya Mjini  ambapo yaliripotiwa matukio 18.

 

Mtakwinu huyo amefahamisha kuwa matukio hayo tayari yameshachuliwa hatua ambapo matukio 92 yapo chini ya uangalizi wa Polisi, mamne (4) yapo  kwa OfisiMkurugenzi wa Mashtaka na tukio moja(1) lipo Mahakamani.

 

Nae Mrakib  Msaidizi wa Jeshi la Polisi ambae ni Mkuu wa kitengo cha Takwimu Makao Makuu ya Jeshi la Polisi Zanzibar Ramadhan Himid amesema vitendo vya udhalilishaji nchini bado ni mbaya hivyo ameiomba jamii kushirikiana na Jeshi la Polisi kwa kutoa taarifa pindi vinapotokea vitendo hivyo ili kuvitokomeza .

 

“Nawaomba wazazi wenzangu kuwa karibu sana na watoto wetu katika kipindi hiki cha sikukuu kwa kutembea nao pamoja na tusiwaache peke yaoili kuwaepusha na vitendo viovu”, alisema Mrakibu huyo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.