Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe.
Abdallah Ulega akiwa ameshika moja ya aina ya mbuzi wanaozalishwa kwenye Ranchi
ya Mkata iliyopo Wilaya ya Kilosa Mkoani Morogororo mara baada ya kufanya ziara
ya kikazi ya siku moja katika ranchi hiyo na kuagiza ranchi hiyo kuendeleza
uzalishaji wa mbuzi kwa ajili ya kufuga kibiashara. (Picha na Edward Kondela, Afisa Habari – Wizara ya Mifugo na Uvuvi)
Na. Edward Kondela
Serikali
imesema Ranchi ya mifugo ya Mkata iliyopo Wilaya ya Kilosa Mkoani
Morogoro itakuwa sehemu ya kuzalisha mbuzi kwa wingi kwa ajili ya
mkakati wa kopa mbuzi lipa mbuzi ambao unatarajia kuanza hivi karibuni
lengo likiwa ni kuwa na mbuzi wa kutosha kwa ajili ya soko la nje ya
nchi.
Akizungumza
na uongozi wa ranchi na Wilaya ya Kilosa, wakati wa ziara ya kikazi ya
siku moja katika Ranchi ya Mkata, Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe.
Abdalllah Ulega amesema ni muhimu kuangalia namna bora ya kufanya
ufugaji wa kibiashara katika ranchi hiyo.
Amesema
serikali imechagua Ranchi ya Mkata kuwa kituo cha kuzalisha mbuzi kwa
wingi ambacho watakuwa wanasambaza katika maeneo mbalimbali nchini.
"Tutakayempa
tutataka tujue yupo wapi na ana mbuzi wangapi ili tuwatambue na
tuwaingize katika mfumo wetu wa takwimu za kibiashara ili iwapo tunapata
mteja wa kilo 50 kwa mwezi kweli tuwe na uhakika wa kupata kilo hizo 50
kwa mwezi.” Amesema Mhe. Ulega
Kutokana
na mkakati huo wa kopa mbuzi lipa mbuzi mahitaji ya mbuzi yatakuja kuwa
makubwa nchini hivyo ameitaka ranchi hiyo kuzalisha mbuzi kwa wingi ili
kuweza kutosheleza soko la ndani na nje ya nchi.
Aidha
Mhe. Ulega amesema wafugaji wa mbuzi wafuge kibiashara ili kuweza
kutimiza vigezo na masharti ya wateja wa kimataifa kama nchini hizo na
kutolea mfano wa nchi za uarabuni ambazo wanataka mbuzi wenye uzito wa
kilo kati ya 8 hadi 10 ambao hawajakomaa sana.
Kwa
upande wake Meneja wa Ranchi ya Mkata Bw. Oscar Magete amesema ranchi
ilianzishwa na serikali kwa madhumuni ya kuendeleza na kueneza ufugaji
bora wa mbuzi, kondoo na ng'ombe ambapo ranchi hiyo kwa sasa ina mbuzi
609 kondoo 116 na ng'ombe 47.
Katika
hatua nyingine Naibu Waziri Ulega ametembelea kiwanda cha kuzalisha
chanjo cha Nobel Vaccine Bioscience (NOVABI) kilichopo Mkoani Morogoro
kinachozalisha chanjo aina ya Tatu Moja kwa ajili ya ya mdondo, ndui ya
kuku na mafua ambayo yanaathiri mfumo wa upumuaji na yamekuwa chanzo
kikuu cha vifo vya kuku na kuwatia hasara wafugaji.
Akiwa
kiwandani hapo Naibu Waziri Ulega ameelekeza chanjo hiyo ya kipekee
isambazwe maeneo mbalimbali nchini hususan vijijini ambapo kuna wafugaji
wengi wa kuku wa kienyeji ili waweze kuipa mifugo yao chanjo kuondokana
na hasara ambayo wamekuwa wakipata ya kuku kufa kutokana na magonjwa
hayo.
Ameongeza
kuwa ni vyema uongozi wa wizara kuhakikisha chanjo mbalimbali
zinazozalishwa ndani na nje ya nchi zinawafikia walengwa hususan waliopo
vijijini ili waweze kufuga kibiashara na waweze kunufaika kupitia
mifugo yao.
No comments:
Post a Comment