Habari za Punde

Ziara ya Kikazi Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Mary Masanja Katika Mji Mkongwe wa Mikindani Mtwara leo.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) (kushoto) akimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Mhe. Dunstan Kyobya (kulia) akitoa maelezo kuhusu ramani ya eneo la Mji Mkongwe Mikindani alipotembelea Makumbusho yaliyo katika eneo la Mji Mkongwe Mikindani katika Manispaa ya Mtwara leo. Katikati ni Mhifadhi Mkuu, Mji Mkongwe Mikindani, Paul Ndahani.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) (wa pili kulia) akichota maji kwenye Kisima cha Asili cha Haikata-Mikindani kinachotumika na wenyeji kwa ajili ya kutambika ili kujibiwa maombi yao, wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua eneo la Mji Mkongwe Mikindani katika Manispaa ya  Mtwara leo. Wanaoshuhudia ni Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Mhe. Dunstan Kyobya (wa tatu kulia), Mjumbe wa Kamati ya Magofu Trade Aid, Alhaji Liloko (kulia) pamoja na baadhi ya watendaji kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii,  Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) na Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania ( TAWA).
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) akitoka kwenye Nyumba ya Mwalimu Nyerere iliyo katika eneo la Mji Mkongwe Mikindani, alipofanya ziara ya kikazi ya kukagua eneo hilo kwa ajili ya kuliboresha katika Manispaa ya Mikindani leo. Wengine ni Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Mhe. Dunstan Kyobya na baadhi ya watendaji kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii, Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) na Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA).
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) (wa tatu kulia) akimsikiliza Mhifadhi Mkuu, Mji Mkongwe Mikindani, Paul Ndahani (kulia) akitoa maelezo kuhusu Nyumba ya Mwalimu Nyerere wakati wa ziara ya kikazi ya kukagua eneo la Mji Mkongwe Mikindani katika  Manispaa ya Mikindani leo. Wengine ni Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Mhe. Dunstan Kyobya (, wa pili kushoto), Mjumbe wa Kamati ya Magofu Trade Aid, Alhaji Liloko (wa kwanza kushoto) na baadhi ya watendaji kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii, Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) na Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA).
                                                                 Picha na Happy Shayo

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.