Habari za Punde

Ziara ya Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mkoani Lindi Mhe.Mary Masanja.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii ,Mhe. Mary Masanja (Mb) akichuma gamba la Mti wa Nyerere unaopatikana katika Shamba la Miti Rondo alipokuwa akikagua shamba hilo katika ziara yake ya kikazi leo Mkoani Lindi.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii , Mhe. Mary Masanja (Mb) akimsikiliza Mhifadhi Mkuu, Hifadhi ya Mazingira Asilia Rondo, Richard Baltazar (kulia) akitoa maelezo kuhusu Hifadhi ya Mazingira Asilia Rondo alipokuwa akikagua shamba la miti Rondo katika ziara yake ya kikazi leo Mkoani Lindi.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii , Mhe. Mary Masanja (Mb) akimwagilia mti wa kumbukumbu alioupanda wakati wa ziara yake ya kikazi katika Ofisi za Wakala wa Huduma za Miti (TFS) Shamba la Miti Rondo leo Mkoani Lindi. Kushoto ni Mkuu wa Kanda ya Kusini wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania, Manyisye Mpokigwe

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii , Mhe. Mary Masanja (Mb) akizungumza na wanachi wa Kijiji cha Rondo katika Halmashauri ya Wilaya ya Lindi katika ziara yake ya kikazi ya kusikiliza kero za wananchi ambapo amewataka wananchi kuendelea kuhifadhi mazingira ili kuendeleza utalii wa eneo hilo Mkoani Lindi leo.

 

 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.