Habari za Punde

Haji Manara Awa Kivutio, Ashukuru Yanga Kwa Kumpokea

Manara alimfunga kamba za viatu Kiungo mahiri wa Yanga Feisal Salum ‘ Fei Toto’ na kumsifia kwa uwezo wake mkubwa uwanjani.

Na Zainab Nyamka, Michuzi TV

Msemaji wa Yanga Haji Sunday Manara amewashukuru Mashabiki wa Yanga kwa kumpokea na kumkubali kama msemaji wao mpya.

Akitoa maneno hayo, Manara amesema mashabiki na wanachama wa Yanga wamempa heshima na anawaahidi kuwapa furaha katika kipindi chote.

“Najiuliza kwanini baba yangu aliniacha niende kule, Yanga kuna raha na nawaahidi mashabiki wa Yanga kuwapa furaha na nitakuwa nanyi bega kwa bega,” amesema

Manara akiwatambulisha wachezaji wa Yanga kabla ya kuanza mechi, amesema msimu huu Yanga ni ya Makombe na sio vingine.

Katika tukio la kipekee, Manara alimfunga kamba za viatu Kiungo mahiri wa Yanga Feisal Salum ‘ Fei Toto’ na kumsifia kwa uwezo wake mkubwa uwanjani.

Aidha, katika sherehe hizo zilizomalizika kwa mchezo wa kirafiki kati ya Yanga na Zanako, Yanga iliwatumia wachezaji wake wapya na kuangalia tathmini ya kila mmoja.

Kwenye mchezo huo Yanga imekubali kichapo cha goli 2-1 goli kwa upande wa Yanga likifungwa na Heritier Makambo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.