Habari za Punde

Kamati ya Fedha, Uchumi na Biashara yakutana kujadili changamoto za Muungano yakutana Dodoma leo

Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba akiongoza kikao cha Kamati ya Fedha, Uchumi na Biashara ngazi ya mawaziri chenye wajumbe kutoka Serikali ya Jamhuri ya Muungano (SMT) na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ).  Mwenyekiti mwenza katika kikao hicho ni Waziri wa Nchi, Afisi ya Rais, Fedha na Mipango Mhe. Jamal Kassim Ali. Kikao hicho kimefanyika leo tarehe 03/08/2021 katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mhe. Selemani Jafo akifuatilia mjadala katika kikao cha Kamati ya Fedha, Uchumi na Biashara ngazi ya mawaziri kikao hicho kimefanyika leo tarehe 03/08/2021 katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma. Kulia ni Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Emmanuel Mpawe Tutuba.

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Mary Maganga (katikati), Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Mohammed Khamis Abdulla (kushoto) na mwakilishi wa Katibu Mkuu Wizara ya Nishati Bw. Haji Janabi wakifuatilia mjadala katika kikao cha Kamati ya Fedha, Uchumi na Biashara ngazi ya mawaziri. Kikao hicho kimefanyika leo tarehe 03/08/2021 katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma.

Baadhi ya Makatibu Wakuu kutoka Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wakifuatilia mjadala katika kikao cha Kamati ya Fedha, Uchumi na Biashara ngazi ya mawaziri kikao hicho kimefanyika leo tarehe 03/08/2021 katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma.

Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba akiongoza wajumbe wa Kikao cha Kamati ya Fedha, Uchumi na Biashara ngazi ya mawaziri kumuombea aliyekuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Elias Kwandikwa aliyefariki jana.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.