Habari za Punde

Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo akagua miradi ya ajira kwa vijana mjini Ole

MWENYEKITI wa kikundi cha Riziki Haina Mja cha Mjini Ole Omar Aminia, akitoa maelezo kwa viongozi Mbali Mbali wa Serikali, akiwemo katibu Mkuu Wizara ya Habari Vijana Utamaduni na Michezo Zanzibar Fatma Hamad Rajab na Mkuu wa JKU Zanzibar Kanali Makame Abdalla Daima, juu ya ufanyaji kazi wa visima vya maji na Green House zilizojengwa na jeshi hilo, kupitia mradi wa ajira kwa vijana.

KATIBU Mkuu Wizara ya Habari Vijana Utamaduni na Michezo Zanzibar Fatma Hamad Rajab, kulia ni mkuu wa JKU Zanzibar kanali Makame Abdalla Daima, wakizindua zoezi la uvunaji wa Vitunguu Maji katika kikundi cha Rizi Haina Mja cha mjini Ole, wakati wa ziara ya kukagua changamoto za visima vya maji na Green House zilizojengwa na JKU.

KATIBU Mkuu Wizara ya Habari Vijana Utamaduni na Michezo Zanzibar Fatma Hamad Rajab, kulia ni mkuu wa JKU Zanzibar kanali Makame Abdalla Daima, katibu Mtendaji baraza la Vijana Zanzibar Salum Issa Ameir, wakiwa wameshika vitunguu maji baada ya kuzindua, katika kikundi cha Riziki haina mja cha Mjini Ole, wakati wa ziara ya kukagua changamoto za visima vya maji na Green House zilizojengwa na JKU.

KATIBU Mkuu wizara ya Habari Vijana Utamaduni na Michezo Zanzibar Fatma Hamad Rajab, akitoa maelezo juu ya mradi wa ajira kwa vijana uliohusisha uchimbaji wa Visima na Ujenzi wa Green House Uliofanya na JKU, hatimae visima hivyo vimeshindwa kutoa maji kama ilivyotarajiwa, katika ziara hiyo walifuatana na mkuu wa JKU Zanzibar Kanali Makame Abdalla Daima.

KATIBU Mtendaji Baraza la Vijana Zanzibar Salum Issa Ameir, akitoa maelezo kwa Mkuu wa JKU Zanzibar Kanali Makame Abdalla Daima, juu ya malengo ya vijana baada ya kuona wamechimbiwa visima vya maji na Ujenzi wa Green House, jambo ambalo limerudisha nyuma jitihada zao kufuatia visima hivyo viliyojengwa na JKU kutokuwa na Maji.

(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.