Habari za Punde

NGOs ZINAZOKIUKA KATIBA ZAO ZAONYWA

 Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Mwanaidi Ali Khamis akikabidhi vifaa vya kunawia mikono kwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wikaya ya Tu duru, Hairu Hemedi Musa kwaajili ya baadhi ya Shule ya Sekondari ziliyopo Wilayani Tunduru Mkoani Ruvuma.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Mwanaidi Ali Khamis akikabidhi vifaa vya kunawia mikono kwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wikaya ya Tu duru, Hairu Hemedi Musa kwaajili ya baadhi ya Shule ya Sekondari ziliyopo Wilayani Tunduru Mkoani Ruvuma.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Mwanaidi Ali Khamis akiangalia moja ya mashine ya kubangua korosho inayotumiwa na vikundi cha Wanawake Wajasirimali Wilayani Tunduru mkoani Ruvuma.
 Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Mwanaidi Ali Khamis akikata utepe kuzindua mashine za kubangua korosho zilizotolewa na Shirika la Viwanda vidogo SIDO Mkoa wa Ruvuma kwa vikundi cha Wanawake Wajasirimali.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Mwanaidi Ali Khamis akiangalia bidhaa za wanawake wajasirimali katika Wilaya ya Tunduru Mkoani Ruvuma.

Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WAMJW

Na Mwandishi Wetu, Tunduru 

Serikali imesema haitofumbia macho Shirika lolote Lisilo la Kiserikali litakalofanya kazi kinyume na Katiba zao na dhumuni la Shirika husika.


Agizo hilo limetolewa na  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Mwanaidi Ali Khamis alipofanya ziara katika Wilaya ya Tunduru Mkoani Ruvuma kukagua shughuli mbalimbali za Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Wilayani humo.


Naibu Waziri Mwanaidi amesisitiza kuwa lengo la Mashirika Yasiyo ya Kiserikali ni kusaidia pale ambapo Serikali haijafika katika kutoa huduma kwa jamii na sio vinginevyo.


"NGOs hizi zinasajiliwa kwa mujibu wa Sheria sasa niziombe tu zifanye kazi kwa kuzingatia Sheria na taratibu zilizopo hatutofumbia macho ukiukwaji wowote wa Sheria na taratibu" alisema Mhe. Mwanaidi


Aidha ameongeza kuwa zipo changamoto nyingi katika jamii ikiwepo vitendo vya ukatili wa kijinsia hasa mimba za utotoni ambazo zimekuwa zikikatisha ndoto za watoto wa kike walio wengi katika meneno mbalimbali nchini.


Kwa upande wake, Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Tunduru ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo Mhe. Dkt. Julius Kenneth Ningu amesema watahakikisha Mashirika Yasiyo ya Kiserikali yanayofanya kazi katika Wilaya ya Tunduru na Mkoa kwa ujumla yanafanya kazi kwa kuzingatia Sheria na taratibu zilizopo.


"Tutahakikisha NGOs zinafuata Sheria na zinafanya kazi kwa mujibu wa usajili wao na kuwanufaisha wananchi" alisema Dkt. Ningu


Ameongeza kuwa Wilaya itasimama vizuri katika kuhakikisha inawachukulia hatua wanaosababisha kuwepo kwa mimba za utotoni


Akizungumza Mratibu wa Mradi wa Afya Mama na Mtoto Katibu wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Masasi Phares Lihewe amesema mradi huo umechangia katika kutoa elimu na vifaa vya kunawa mikono ikiwa ni hatua za kujikinga na UVIKO 19 katika Shule mbalimbali za Sekondari Wilayni Tunduru.


Katika ziara yake Wilayani Tunduru Naibu Waziri Mwanaidi amekabidhi vifaa vya kunawa mikono kwa baadhi ya Shule za Sekondari Wilayani humo na kukagua shughuli za kiuchumi za wanawake wajasirimali.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.