Habari za Punde

Kikao cha kujadili suala zima la heshima kwa wanazuoni chafanyika ukumbi wa Mikutano Masjid Jamiu Zinjibari

Katibu Mkuu wa Marafiki wa Zanzibar Aboubakar Kabogwi akizungumza katika kikao cha kujadili suala zima la heshima kwa wanazuoni na kuwaombea dua Viongozi wakuu wa  Nchi , kilichofanyika Ukumbi wa Mikutano Masjid Jamiu Zinjibar huko Mazizini Mjini Unguja.

Profesa Issa Haji Zidi akichokoza mada katika kikao cha kujadili suala zima la heshima kwa wanazuoni na kuwaombea dua Viongozi wakuu wa  Nchi kilichofanyika Ukumbi wa Mikutano Masjid Jamiu Zinjibar Mazizini Mjini Unguja.

Mkurugenzi Idara ya Fatwa Ofisi ya Mufti Zanzibar Sheikh Khamis Gharib akichokoza mada katika kikao cha kujadili suala zima la heshima kwa wanazuoni na kuwaombea dua Viongozi wakuu wa  Nchi kilichofanyika Ukumbi wa Mikutano Masjid Jamiu Zinjibar Mazizini Mjini Unguja.

Dr.Muhidini akichangia mada ya   heshima kwa wanazuoni na kuwaombea dua Viongozi wakuu wa  Nchi katika kikao kilichowashirikisha Maulamaa na Wanazuoni huko Masjid Jamiu Zinjibar Mazizini Mjini Unguja.

Mjumbe kutoka Braza la Maulama Sheikh Khamis Abdul-hamid akichangia mada ya   heshima kwa wanazuoni na kuwaombea dua Viongozi wakuu wa  Nchi katika kikao kilichowashirikisha Maulamaa na Wanazuoni huko Masjid Jamiu Zinjibar Mazizini Mjini Unguja.

Katibu Mkuu wa Mufti Sheikh Khalid Ali Mfaume akizungumza katika kikao cha kujadili suala zima la heshima kwa wanazuoni na kuwaombea dua Viongozi wakuu wa  Nchi , kilichofanyika Ukumbi wa Mikutano Masjid Jamiu Zinjibar huko Mazizini Mjini Unguja.

Sheikh Abdalla Hadhar akichangia mada ya   heshima kwa wanazuoni na kuwaombea dua Viongozi wakuu wa  Nchi katika kikao kilichowashirikisha Maulamaa na Wanazuoni huko Masjid Jamiu Zinjibar Mazizini Mjini Unguja.
Sheikh Ramadhan Suleiman soraga akichangia mada ya   heshima kwa wanazuoni na kuwaombea dua Viongozi wakuu wa  Nchi katika kikao cha elimu cha Wanazuoni na Maulamaa kilichofanyikaUkumbi wa Mikutano Masjid Jamiu Zinjibar Mazizini Mjini Unguja.
Mufti Mkuu wa Zanzibar akizungumza na Wanazuoni pamoja na Maulamaa (hawamo pichani) katika kikao cha kujadili suala zima la heshima kwa wanazuoni na kuwaombea dua Viongozi wakuu wa  Nchi , kilichofanyika Ukumbi wa Mikutano Masjid Jamiu Zinjibar huko Mazizini Mjini Unguja.
 

Na Issa Mzee   - Maelezo 16/08/2021

Matumizi ya busara, hekima na utii wa viongozi ni miongoni mwa mambo ya msingi ambayo yanahitaji kuenziwa ili kuhakikisha amani inadumu visiwani Zanzibar.

Kauli hiyo imetolewa na Mufti wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi, katika Msikiti wa Jamiu Zinjibar Mazizini, katika kikao maalumu kilichoandaliwa na Ofisi ya Mufti kilicholenga kujadili umuhimu wa kuwaheshimu wanazuoni na kuwaombea dua viongozi nchini.

Amesema tofauti ya madhehebu na khitilafu katika masuala mbalimbali ya dini yalikuwepo zamani lakini kutokana na busara, hekima na kuheshimiana kwa wanazuoni kumeiweka Zanzibar katika hali ya ustaarabu.

Alieleza kuwa, matumizi ya maneno mazuri na kuacha kulaumiana na kuwazungumza vizuri wanazuoni ni mambo yenye faida kubwa katika jamii hivyo maulamaa lazima watiiwe.

“Matumizi ya busara yanahitajika kila sehemu katika jamii hasa katika dini yetu ya Kiislamu ipo haja kwa wanazuoni kupendana, kuungana na kuweka mioyo yao safi kila wakati ili kuepusha mitafuruku nchini”, alisema Mufti.

Akizungumzia umuhimu wa kuwaombea dua viongozi katika ngazi mbalimbali nchini, Sheikh Kabi alisema ni vyema kumuombea dua kiongozi wa ngazi yoyote ile ili wapate kuleta maendeleo katika majukumu yao.

“Viongozi ndio moyo wananchi, akituongoza vizuri jamii itafaidika na akifanya tofauti jamii itakosa maendeleo hivyo ni muhimu sana kuwaombea dua ili watuongoze vizuri na tuwaombee endapo watakosea  Mungu awaongoze”, alifahamisha Mufti wa Zanzibar.

Aidha alieleza kuwa uadilifu wa kiongozi ni muhimu kwa maendeleo ya taifa hivyo ni vyema kuwaombea dua ili waweze kuinufaisha jamii kwa uadilifu.

Akitoa mchango kuhusu umuhimu wa kuwaheshimu wanazuoni Sheik Fadhil Soraga alisema ni vyema kwa kila mwanzuoni kuwa mpole na kuacha tabia ya kujikweza ambayo hupelekea matumizi ya maneno mabaya baina yao.

Alisistiza kwamba kauli nzuri, sahihi na zisizo na khitilafu ni jambo la msingi na kuachana na utoaji wa lugha ambazo husababisha migogoro na mifarakano katika jamii.

Sheikh Soraga alieleza kuwa, mongoni mwa sababu zinazoleta mitafaruku baina ya wanazuoni ni ufahamu mbaya wa baadhi ya mambo ya dini na kukosa hekima pamoja na kutokuheshimiana baina yao.

Aliwataka wanazuoni kuimarisha maadili ya dini na ustaarabu wa kiislamu ili kuleta umoja nchini.

Nae mjumbe wa Baraza la Maulamaa Sheikh Khamis Abdallah, alisema kusoma nje ya nchi isiwe sababu ya kufarikiana baina ya wanazuoni wa dini ni vyema kila moja kuifanyia kazi elimu yake kwa usahihi ili iweze kuinufaisha jamii.

Alieleza kuwa kufarikiana baina ya wanazuoni hivi sasa kunachangiwa kwa kiasi kikubwa na ubinafsi wa mtu na sio sababu ya dini hivyo ni vyema kila mwanazuoni kufuata maelekezo ya dini kikamilifu.

Sheikh Kamis aliwashauri wanazuoni kutoa dalili za wazi na sahihi  kwa mujibu wa Qur-ani na sunna na sio kuzua au kuleta mambo yasio na uthibitisho katika dini ili kuiweka  jamii katika njia ya haki.

Mapema Mkurugenzi wa Idara ya Fatwa kutoka Ofisi ya Mufti Zanzibar Sheikh Khamis Gharib alisema viongozi wana haki ya kuombewa dua kwa mujibu wa mafundsiho ya dini.

Aliisisitiza jamii kuwatii viongozi wao katika hali ya wepesi na uzito ili kuiweka jamii katika hali ya amani.

Alifahamisha kuwa kuwatii, kuwapenda na kuwaombea dua ya kheri sio jambo baya bali  ni kuleta manufaa katika dini na taifa.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.