Habari za Punde

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan Awasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Akitokea Nchini Malawi.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Phillip Mpango mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume wakati akitokea nchini Malawi leo 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akisalimiana na viongozi mbalimbali mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume wakati akitokea nchini Malawi leo. 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akizungumza na Rais Mstaafu wa Malawi Bi. Joyce Banda Lilongwe nchini Malawi. Rais Mstaafu Joyce Banda alifika Lilongwe kuzungumza na   kumpongeza Rais Mhe. Samia kwa kuwa Rais wa kwanza Mwanamke nchini Tanzania.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiagana na Rais Mstaafu wa Malawi Bi. Joyce Banda mara baada ya mazungumzo yao yaliofanyika Lilongwe nchini Malawi.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiondoka katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kamuzu mara baada ya kushiriki Mkutano wa 41 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) uliomalizika leo tarehe 18 Agosti katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Bingu uliopo Jijini Lilongwe nchini Malawi.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.