Na Miza Kona Maelezo Zanzibar 13/08/2021.
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeanza kutoa vitambusho maalum vya uthibitisho wa chanjo ya Uvico 19 kwa wale wanaokamilisha dozi ya chanjo hiyo.
Akitoa taarifa ya serikali kuhusiana na Upatikanaji wa Vitambusho vya Chanjo ya Uvico 19 kwa waandishi wa habari Waziri wa Afya, Ustawi wa Jami, Jinsia na Watoto Mhe. Nassor Ahmed Mazrui, amesema serikali inatoa kadi kwa mwananchi yetote atakaekamilisha dozi ya chanjo ya covid 19 kwa ajili ya uthibitisho popote anapokwenda.
Amesema kitambulisho hicho chenye ubora ambacho kitakuwa na taarifa kamili za muhusika ,kitatambulika na kutumika katika mataifa mbalimbali bila ya kupata usumbufu au vikwazo vyovyote .
Amefahamisha kuwa kitambuisho hicho sio lazima lakini ni muhimu kwa wale waliokamilisha dozi, ambacho kinapatikana Wirara ya Afya katika kitengo cha Chanjo baada ya kukamilisha hatua za uchomaji kwa gharama y a sh. 20,000 .
“Kadi hii itakuwa ni kielelezo na uthibisho kuwa umechanja na itakusaidia kwa shughuli binafsi au za Serikali kwa wafanyabiashara , wafanyakazi na wanaosafiri Nje ya Nchi , pia katika mikutano ya kimataifa utaonesha kuwa tayari una kinga”, ameeleza Waziri Mazrui.
Waziri Mazrui amesema kuwa,Sserikali inatoa kitambulisho kwa gharama nafuu kwa wananchi wake ili wapate kufaidika na huduma hiyo pamoja na kuepuka kupata gharama kubwa wanapokihitaji katika nchi nyengine.
Amefahmisha kuwa gharama za ulipaji kwa ajili kitambulisho hicho zitalipwa kwa njia ya banki ya PBZ kupitia namba 0748946002.
Akitoa ufafanuzi kuhusiana na madhara yaliyotokea kwa wale waliochanja chanjo COVID 19 Waziri Mazrui amesema kuwa hakuna tatizo lililojitokeza kutokona na chanjo hiyo, kwa mtu yeyote kati ya watu 10,000 waliochanjwa.
Nae Mkurugenzi Mtendaji Wakala wa Serikali Mtandao Zanzibar Said Seif Said amesema kitambulishi hicho kipo imara, kina taarifa zote za muhusika pamoja na taarifa za kiafya ambazo zitakuwa na usalama mkubwa.
No comments:
Post a Comment