Fransiska Camilius Clement akichangia kuhusu umuhimu wa wanawake na kushika nafasi za uongozi
Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya siku tatu kuhusu umuhimu wanawake kushiriki kwenye uongozi na demokrasia
Mkurugenzi wa Chama cha Wanasheria Wanawake Zanzibar (ZAFELA )Jamila Mahmoud Juma amesema ipo haja kwa jamii kufahamu umuhimu wa uongozi bora na demokrasia katika maeneo yao wanayoishi ili kujenga jamii yenye usawa.
Ameyasema hayoa ofisini kwake kwa mchina mjini Unguja kufuatia mafunzo ya siku tatu kwa vijana 60 kutoka wilaya zote za Unguja ambao watakua na kazi ya uhamasishaji katika jamii kuhusu umuhimu wanawake kushiriki kwenye uongozi na demokrasia.
Alisema kundi hilo la vijana watakua na kazi ya kuwaelimisha wengine kwenye jamii sambamba na kuhamaisha wanawake kushiriki kwenye nafasi za uongozi.
Alieleza kuwa kupitia elimu hio anaamini wanawake wengi watajitokeza kuwania nafasi za uongiozi au hata kuhakikisha wanachagua viongozi wazuri na wenye manufaa kwa maslahi yao.
Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo walisema mafunzo hayo yamekuja wakati muafaka na wanaamini watayafanyia kazi inavostahiki.
Awali mratibu wa mradi wa ushirikishaji wanawake katika uongozi TAMWA-ZNZ Salma Amir Lusangi alisema mradi huo unalenga kuwafikia wanawake 6000 ili waweze kudai haki zao katika uongozi.
Amewataka washirki wa mafunzo hayo waelewe kwamba wana jukumu kubwa la kuwahamisisha wanawake kudai haki zao za uongozi ikiwemo kisiasa,kiuchumi na kijamii.
Kwa upande wake Fransiska Camilius Clement alisema uwepo wa nafasi maalumu za uongozi kwa wanawake ni kitu ambacho hakipasawi kuondolewa kwa kuwa kunatoa fursa kwa wanawake wengi kujiadaa.
Katika hatua nyengine alisema kuna haja ya jamii kuwaunga mkono wanawake wanaojitokeza kugombea nafasi mbali mbali za uogozi kwani wanawake ni watu waliojaaliwa na huruma kuliko wanaume hivyo ni rahisi kutekeleza majukumu yao.
No comments:
Post a Comment