Habari za Punde

Waziri Mkuu Mhe.Majaliwa Ameweka Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Hospitali ya Wilaya Karangwe.

 

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiweka jiwe la msingi la  Hospitali ya Wilaya ya Karagwe, Septemba 19, 2021. Kulia ni Naibu Waziri TAMISEMI (Elimu), David Silinde.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua ujenzi wa Hospitali ya wilaya ya Karagwe baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wake akiwa katika ziara  ya kikazi Mkoa wa Kagera, Septemba 19, 2021. Kushoto ni Naibu Waziri TAMISEMI (Elimu), David Silinde.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua marumaru zilizowekwa kwenye Wodi ya Wazazi katika  Hospitali ya wilaya ya Karagwe na baada ya kutorishishwa na ubora wake aliamuru ziondolewe na ziwekwe nyingine zenye viwango vinavyofanana na pesa iliyotolewa na Serikali. Alikuwa katika ziara ya kikazi mkoani Kagera.

Marumaru zisizo na  viwango vinavyokubalika serikalini ambazo zimewekwa kwenye  sakafu ya Wodi ya Wazazi katika Hospitali ya wilaya ya Karagwe. Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amegiza ziondolewe na badala yake ziwekwe marumaru zenye ubora unaokidhi viwango vya Serikali. Mheshimawa Majaliwa alitoa maagizo hayo wakati alipokagua ujenzi wa hospitali hiyo akiwa katika ziara ya Mkoa wa Kagera, Septemba 19, 2021.
 (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.