Habari za Punde

Mwenyekiti wa Sensa ya Watu na Makaazi Mhe Kassim Majaliwa Aongoza Kikao Cha Kamati ya Kitaifa ya Sensa Tanzania.

Mwenyekiti wa Kamati ya Taifa ya Sense ya Watu na Makaazi ambae pia ni Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akiwapongeza Kikao cha Wajumbe wa Kamati ya Sensa Tanzania kwa kazi nzuri wanayoendelea kuifanya katika kufanikisha zoezi la Sense ya Watu na Makaazi Tanzania na (kulia) Mwenyekiti Mweza wa  Kamati ya Sensa na Makaai  ambae pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman Abdulla.

Wajumbe wa Kamati kuu ya Taifa ya sense ya watu na makaazi wakimskiliza Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Kassim Majaliwa wakati akiendesha kikao cha kwanza cha kamati hiyo.
Mwenyekiti wa Kamati ya Taifa ya sense na watu na Makaazi Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa  akiagana na Mwenyekiti Mwenza ambae pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zaznibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla mara baada ya kumaliza kikao hicho kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere Convesion Centre Jijini Dar es- Salam

Na.Kassim Abdi.OMPR.

Wajumbe wa Kamati kuu ya sense ya watu na makaazi wamekutana katika kikao cha kwanza,  kwa lengo la kujenga uwelewa wa pamoja, juu ya zoezi la sense ya watu na makaazi, linalotarajiwa kufanyika mwezi Agosti 2022.

Akifungua kikao hicho cha kwanza Mwenyekiti wa Kamati kuu ya Taifa ya sensa ya watu na makaazi Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaaliwa Majaaliwa amewapongeza watendaji wa kamati hiyo pamoja na watendaji kutoka Ofisi za Takwimu kwa kazi nzuri wanaoyoendelea kuifanya ya kujenga uwelewa kwa wananchi juu ya zoezi la sense ya watu na makaazi.

Amesema kuwa, lengo kuu la kikao hicho ni kuwakutanisha pamoja watendaji wa pande zote mbili za Jamuhuri  ya Muungano wa Tanzania ili kuwajengea uwelewa wa pamoja katika kufanikisha zoezi  la sense ya watu na makaazi  kwa mafanikio zaidi.

Waziri Mkuu Kassim Majaaliwa amesema serikali itaendelea kuwashirikisha viongozi wa dini katika kujenga uwelewa huo wa pamoja kwa lengo la kufuta fikra potofu zinazosambazwa na baadhi ya watu wasiokuwa na utaalamu juu ya zoezi hilo.

Kabla ya kuaghirisha kikao hicho Mwenyekiti mwenza wa Kamati kuu ya sense ya watu na makaazi ambae pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla amewahakikishia wajumbe wa kamati hiyo kuwa serikali zote mbili ziataendelea kutoa ushirikiano kwa watendaji wa zoezi hilo ili kufikia azama ya serikali ilioikusudia.

Makamu wa Pili wa Rais amewataka watendaji kutoka ofisi zote za Takwmu kwenda kutekeleza utaalamu wao kwa vitendo ili kuonesha sura halisi kuwa sense inayotarajiwa kufanyika itazingatia mifumo mipya ya kidijital kwa kulinganisha na sense zilizopita.

Wakiwasilisha taarifa fupi Katibu Mkuu waizara ya Fedha na Mipango Ndugu Emaul Tutuba na Katibu Mkuu Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Fedha Mipango Dk. Juma Malik Akili wamsema lengo kuu la sense ya watu na makaazi inalenga kupata takwimu za msingi zitakazosaidia kutunga sera, kupanga na kufuatilia mipango ya maendeleo kwa ajili ya wananchi.

Wameleza kuwa, sense ya sita inayotarajiwa kufanyika nchini inatarajiwa kuwa ya kipekee kutokana na matumizi ya ubunifu na matumizi ya Teknolojia ikilinganishwa na sense zilizopita.

Wamefafanua kwamba, serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ipo katika hatua za awali ikiwa tayari imeshajipanga vyema kwa zoezi la sense ya majaribio ikiwa  vitongoji vilivyomo katika jumla ya wilaya 35 kati ya wilaya 139 sawa na asilimia 25 mipata yake imehakikiwa na kutengwa kama maeneo ya kuhesabia watu.

Akizungumzia juu ya mataarisha ya sense ya majaribio Katibu Mkuu Juma Malik Akili amesema kazi ya utengaji wa maeneo ya sense ya majaribio tayari imekamilika ambapo jumla ya maeneo Kumi ya kuhesabu watu ikiwa Unguja maeneo Sita na kwa upande wa Pemba maeneo manne yamechaguliwa.

Ameleza kuwa, Pia serikali kupitia Ofisi ya mtakwimu Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (OCGS) imeendesha mafunzo kwa makarani  na wasimamizi wa sense ya majaribio kutoka katika sehemu husika ikiwajumuisha wataalamu kutoka OCGS, waratibu wa sense wa wilaya na Mikoa kupita maeneo ambayo yamechaguliwa.

Kikao hicho kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere Convesion Centre   Jijini Dar es Salam kimewakutanisha waheshimiwa mawaziri na Makatibu wakuu kutoka pande zote mbili za Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.