Na RAYA
HAMAD – OMKR.
Washiriki
wa mafunzo ya uwasilishaji michango ya wanachama wa Mfuko wa hifadhi ya jamii
ZSSF kwa njia ya kielektroniki kutoka Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais
wametakiwa kuwa na mashirikiano ya pamoja kwa kuupokea na kuuzowea mfumo wa
kielektroniki ili taarifa za waajiriwa wake ziendane na michango yao wanayoitoa
Mkurugenzi
uendeshaji na utumishi ndugu Juma Ali Simai ameyasema hayo wakati akifungua
mafunzo ya siku moja yaliyowashirikisha maafisa utumishi, wahasibu na maafisa
tehama wa Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais na taasisi zake kuhusiana na
uwasilishaji michango ya wanachama wa ZSSF kwa njia ya kielektroniki kwenye
ukumbi wa mkutano Migombani
Amewakumbusha
washiriki hao kuwa kuwekwa kwao pamoja katika mafunzo hayo ni kujengwa uwelewa
na kuzidisha uwezo katika majukumu yao kwa
kushirikiana pamoja jambo ambalo
litatoa fursa kwa watendaji hao kusaidiana pale ambapo kutatokea mabadiliko iwe
ya kubadilishwa ofisi ama masuala ya kiutendaji
Aidha
amwasisitiza washiriki hao kukaa na watumishi wote na kuwapa elimu juu ya kile
walichojifunza “hakuna sababu ya mfanyakazi yoyote wa Ofisi hii kubaki nyuma
ama kupitwa na mfumo huu kupitia simu za kiganjani ama komputa hapa ofisini ili
kila mmoja wetu aweze kuona kama kuna mapungufu ama kukosekana taarifa sahihi
za michango yake kupitia simu yake ataweza kufatilia kwa ukaribu na kuweka sawa
taarifa zake “alisisitiza Mkurugenzi Juma
Mkurugenzi
Juma amesema Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais itaendelea kutoa mafunzo kwa
watendaji wake na taasisi zake kwa kila kada kila hali inaporuhusu na kwa
mujibu wa mpango mkakati wa Ofisi hio
Nae meneja
Tehama kutoka ZSSF Bw Ali Haji Ameir amesema mafunzo ya kujenga uelewa ni
muhimu ukizingatia kuwa ZSSF imejipanga vyema na itakapofika mwezi wa Disemba
2021 itakuwa ndio mwisho wa uwasilishaji
michango kwa njia ya kikawaida
iliyozoweleka na badala yake taasisi za Serikali na mashirika binafsi yatalazimika kuwasilisha michango ya
wanachama kwa kufuata mfumo kwa njia ya
kielektroniki
Hivyo
amesisitiza kuwa njia ya kisasa ya mfumo wa kielektroniki ya uwasilishaji
michango ya wanachama wa ZSSF ni rahisi na salama zaidi iwapo muwasilishaji atakamilisha taratibu za
usajili kwa vile kwa kutumia njia ya mfumo wa kielektroniki uwasilishaji michango unaweza ukafanyika muda
wowote
Washiriki
wa mafunzo wamejifunza jinsi ya kuwasilisha michango ya wafanyakazi kwa mfuko wa hifadhi ya jamii ZSSF, maslahi
ya watendaji kuelea kustaafu, namna ya mwanachama mmoja mmoja wa mfuko kupata
taarifa kwa kutumia simu ya kiganjani au komputa.
No comments:
Post a Comment