Habari za Punde

Wananchi 600 Wapatiwa Hati za Miliki za Kimila Wilayani Nzega.

Wananchi wa kata ya sigili wilaya ya Nzega wakiwa katika picha ya pamoja na mkuu wilaya hiyo Acp  Advera Bulimba pamoja na viongozi mbalimbali kutoka ofisi ya makamu wa Raisi waliokaa mstari wa mbele

Na Lucas Raphael,Nzega

Serikali  imewapatia hati  miliki za kimila wananchi 600 katika kata ya sigili wilaya ya nzega mkoani Tabora kwa lengo la kupunguza migogoro ya Ardhi .

Akikabidhi hati hizo kwa wananchi  mkuu wa wilaya ya Nzega Acp Advera Bulimba katika sherehe za kugawa hati za haki miliki za kimila kata ya sigiri katika ofisi ya kata hiyo jana alisisitiza kupunguza migogoro ya mipaka kati wa kijiji na wananchi  .

Alisema kwamba hati za kumiliki ardhi kimila  600 zitatolewa kwa wananchi hao zimegharamiwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na wananchi  walichangia  kiasi cha shilingi 20,000/

Acp advera alisema na  kusisitiza kwa wananchi wa Wilaya ya Nzega kuona umuhimu na kulipa uzito suala la kupima maeneo yao kwani  Hati miliki za Kimila ni ustawi maisha yao.

 “Ikumbukwe kuwa katika kusukuma suala la Hati miliki za kimila katika ilani ya Chama Cha Mapinduzi ili elekeza kuwa mpaka mwaka 2025 maeneo yote yawe yamepimwa nchi nzima.”alisema  Acp advera

Mkuu huyo wa wilaya ya Nzega alisema kwamba Hati miliki za kimila zitawasaidia katika mambo mengi hususani katika suala la kupata mikopo ya kibenki kwa kilimo na Pembejeo.

Acp advera alisema kwamba mradi huu ni kurejesha ardhi iliyoharibika na kuongeza usalama wa chakula ambapo unatekelezwa katika kata ya Sigiri na vijiji vyake.

Alisema kwamba Lengo kuu la mradi ni kuwezesha utunzaji wa mazingira na kuongeza uzalishaji wa chakula ambapo kutachangia moja kwa moja kuboresha mazingira  .

Awali mratibu wa mradi  wa kurejesha ardhi iliyoharibika na kuongeza usalama wa chakula katika maeneo kame ya Tanzania Hassani Mtomekela alisema  mradi unalenga kuboresha usimamizi endelevu na kuwezesha urejeshwaji wa mifumo ikolojia iliyoharibika inayochangia kutoa huduma muhimu za uzalishaji kwenye maeneo ya Ardhi, Maji, Misitu na Bionuai kwa madhumuni ya kuongeza uzalishaji wa chakula.

“Kuendelea kuboresha kilimo hifadhi na rafiki kwa mazingira, hifadhi ya ardhi, hifadhi ya vyanzo vya maji na usimamizi wa mifumo ya nyanda za malisho “alisema alisema Mtomekela   

 Naye kaimu mkurungezi mradi huo kutoka ofisi ya makamu wa Rais mazingira Yubo Kiungo alisema kwamba Mpango wa matumizi bora ya ardhi ni moja kati ya shughuli zilizotekelezwa wakati wa utekelezaji wa mradi wa kurejesha ardhi iliyoharibika na kuongeza usalama wa chakula katika maeneo kame Tanzania katika Halmashauri ya Wilaya ya Nzega.

Alisema kwamba kutafanyika  shughuli zinahusiana na hifadhi kilimo, mbinu bora za kilimo rafiki kwa mazingira, uvunaji wa maji ya mvua, vitalu vya miti na usimamizi endelevu wa misitu

Alisema kwamba hadi kukamilisha kazi hiyo serikali imetumia kiasi cha shilingi milioni 85.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.